Habari Mseto

Katibu akiri serikali haijatuma pesa za matumizi shuleni

January 8th, 2024 1 min read

NA MWANGI MUIRURI 

KATIBU mkuu katika wizara ya Elimu Dkt Belio Kipsang’ amekiri kwamba serikali haijatuma pesa za kugharamia elimu katika shule nchini.

Hii ni licha ya serikali kutangaza kwamba ilituma Sh31.3 bilioni wiki iliyopita katika akaunti za shule.

Bw Kipsang’ sasa anasema pesa hizo zitatumwa kati ya leo Januari 8 na Januari 10, 2024, huku shule zikiwa tayari zimefunguliwa.

Hali hii imezua hisia kali na shutuma katika sekta ya elimu, wazazi wakilazimika kugharamia matumizi ya wanafunzi wao.