Kaunti kuboresha barabara zinazoelekea kwa mbuga za wanyama kuinua utalii

Kaunti kuboresha barabara zinazoelekea kwa mbuga za wanyama kuinua utalii

NA WINNIE ATIENO

SERIKALI ya Kaunti ya Taita Taveta imepanga kukarabati barabara zinazoelekea kwa mbuga za wanyamapori ili kuimarisha utalii.

Akiongea kwenye mkutano wa wawekezaji wa utalii wa mbuga za wanyamapori na wadau wa mazingira kutoka Canada, Naibu Gavana, Bi Christine Kilalo, aliwahakikishia ushirikiano ili kupiga jeki sekta hiyo.

“Tunataka kushirikiana na wawekezaji wa sekta za utalii hasa wale wanaozingatia mazingira na mali asili ili kusaidia wakazi wa Taita Taveta kimapato,” alisema Bi Kilalo.

Mkurugenzi wa Idara ya Michezo, Vijana na Utamaduni, Bw Wallace Mwaluma, alisema serikali hiyo inanakili sehemu zote za utamaduni ili kuvutia watalii kuzuru maeneo hayo.

  • Tags

You can share this post!

Wakulima wataka Ruto atimize ahadi ya mradi wa Bura

MWALIMU WA WIKI: Kwa Akinyi ualimu si kazi bali uraibu hasa!

T L