NA COLLINS OMULO
SERIKALI ya Kaunti ya Nairobi imeongeza juhudi za kuwaondoa wafanyakazi hewa katika orodha ya wafanyakazi inaowalipa mishahara.
Ili kutimiza hilo, imeanza mpango wa kuhifadhi maelezo ya wafanyakazi wake wote kwa njia ya kidijitali.
Tayari, kaunti hiyo imetenga Sh10 milioni kuanzisha kadi za kidijitali za wafanyakazi na kuweka mfumo wa kidijitali kuwatambua wafanyakazi wake wote wanaozidi 13,000.
Novemba 2022, Gavana Johnson Sakaja alisema serikali yake ingeanzisha mpango mahsusi kuwaondoa wafanyakazi hewa.