Michezo

KCB, Homeboyz zatinga robo-fainali ya duru ya tano Christie Sevens

August 31st, 2019 2 min read

Na GEOFFREY ANENE

VIONGOZI KCB pamoja na mabingwa watetezi Homeboyz wametinga robo-fainali ya duru ya tano ya raga ya kitaifa ya wachezaji saba kila upande ya Christie Sevens uwanjani RFUEA jijini Nairobi, Jumamosi.

Washiriki wengine ambao wamejikatia tiketi ya kushindania taji msimu huu ukielekea kufika ukingoni ni Menengai Oilers, Mwamba, Nondies, Impala Saracens, Masinde Muliro (MMUST) na Nakuru.

KCB, Mwamba na Nakuru walikamilisha siku ya kwanza ya Christie Sevens kwa kushinda mechi zao zote nayo Nakuru ndiyo klabu nyingine iliyomaliza mechi za makundi bila kupoteza baada ya kuambulia sare moja na ushindi mbili.

Baadhi ya miamba walioteremka kuwania nafasi ya tisa hadi nambari 16 ni Kenya Harlequin, ambao ni wenyeji, na Kabras Sugar.

KCB inaongoza mashindano haya ya duru sita kwa alama 72. Ilishinda duru mpya ya Kakamega Sevens iliyofungua msimu pamoja na Dala Sevens mjini Kisumu. Wanabenki wa KCB wako alama tatu pekee mbele ya washindi wa duru ya Kabeberi na Prinsloo, Mwamba. Siku ya mwisho ya Christie hapo Jumapili inatarajiwa kushuhudia ushindani makali hata zaidi kabla ya duru ya mwisho ambayo ni Driftwood mjini Mombasa mnamo Septemba 7-8.

Matokeo (Agosti 31)

Wanaume

Kundi A

Nondies 10-5 Strathmore Leos, Strathmore Leos 36-14 Egerton Wasps, Mwamba 34-0 Egerton Wasps, Mwamba 24-0 Nondies, Nondies 31-0 Egerton Wasps, Mwamba 14-12 Strathmore Leos

Kundi B

Kenya Harlequin 17-17 Impala Saracens, Kenya Harlequin 32-7 Pirates (Uganda), Impala Saracens 38-5 Pirates (Uganda), Homeboyz 46-5 Pirates (Uganda), Homeboyz 17-12 Kenya Harlequin, Homeboyz 5-17 Impala Saracens

Kundi C

Kabras Sugar 12-19 MMUST, Kabras Sugar 12-7 Blak Blad, Nakuru 19-5 Blak Blad, Nakuru 24-12 MMUST, Nakuru 36-12 Kabras Sugar, Blak Blad 17-17 MMUST

Kundi D

KCB 17-5 Northern Suburbs Cubs, KCB 26-7 Daystar Falcons, Menengai Oilers 29-5 Daystar Falcons, Menengai Oilers 29-21 Northern Suburbs Cubs, KCB 24-5 Menengai Oilers, Northern Suburb Cubs 24-5 Daystar Falcons

Wanawake

Homeboyz 12-12 Mwamba

Impala Saracens 28-0 Northern Suburbs Ladies

Nakuru 10-10 Homeboyz

Northern Suburbs 42-5 Comras

Mwamba 19-19 Nakuru

Impala Saracens 52-0 Comras