Michezo

KCB yatuza timu yake ya raga kwa kugaragaza washindani

October 4th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

TIMU ya raga ya KCB RFC imetuzwa na kampuni ya Kenya Commercial Bank kwa kufanya vizuri katika mashindano ya hivi majuzi.

Timu hiyo ilituzwa kwa kupelekwa nchini Afrika Kusini kwa mazoezi ya kina baada ya kushinda kombe la Kenya Cup mara tatu katika muda wa miaka minne.

Timu hiyo imekuwa Afrika Kusini tangu Septemba 26 na itamaliza mazoezi hayo Oktoba 7, 2018.

Tuzo hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa KCB Joshua Oigara. Katika mazoezi ya mwaka huu, timu hiyo ilitafutiwa wataalam zaidi ambao wamekuwa wakiwasaidia mambo tofauti.

“Tunafurahi sana kwamba timu yetu itafanya mazoezi kwa karibu na wataalamu. Tunajua kuwa utaalam watakaopata watautumia kujitayarishia mashindano ya msimu ujao unaoanza Novemba 2019,” alisema msimamizi wa maslahi ya wateja Job Njiru.