Kebs yapiga marufuku aina 10 za mafuta ya kupikia nchini

Kebs yapiga marufuku aina 10 za mafuta ya kupikia nchini

NA WINNIE ONYANDO

SHIRIKA la Kudhibiti Ubora wa Bidhaa nchini (Kebs) limepiga marufuku kuuzwa kwa aina 10 za mafuta ya kupikia likisema kuwa ni hatari kwa afya.

Mafuta ambayo matumizi yake yamepigwa marufuku kwa muda huku uchunguzi kuhusu ubora wake ukiendelea ni Rina, Fresh Fri yaliyo na mafuta ya tangawizi, Fry Mate, Tilly, Top Fry, Salit, Gold and Pure Olive Gold, Bahari Fry na Postman.

“Mafuta brandi hizo hayafai kwa matumizi kwani ubora wake unatiliwa shaka,” ikasema Kebs.

Mkurugenzi wa Kebs, Peter Kaigwara, alisema shirika hilo lilichukua hatua hiyo kulinda afya ya watumiaji wa mafuta.

  • Tags

You can share this post!

Familia za waliokufa kwenye mauaji ya Wagalla zataka fidia

DOUGLAS MUTUA: Tamaa ya kutajirika haraka imevuruga sifa...

T L