KEFWA kuandalia nyota kutoka Ligi Kuu ya wanawake tuzo ya wanasoka bora Desemba 14

KEFWA kuandalia nyota kutoka Ligi Kuu ya wanawake tuzo ya wanasoka bora Desemba 14

Na GEOFFREY ANENE

Chama cha Maslahi ya Wanasoka wa Kenya (KEFWA) kitaandaa hafla ya kutuza wachezaji bora kutoka Ligi Kuu ya Wanawake kwa mara ya kwanza kabisa wa msimu 2020-2021 mnamo Desemba 14.

Sherehe hiyo itafanyika katika Chuo Kikuu cha Zetech mjini Ruiru katika kaunti ya Kiambu kutoka saa saba mchana hadi saa kumi na moja jioni. Wachezaji walichaguliwa kupitia kura msimu wote wakati wa kuchagua mchezaji bora wa KEFWA wa mwezi. Hafla ya Desemba 14 ni ya kutuza wachezaji 11 bora katika kila nafasi.

Orodha ya kwanza ilijumuisha wachezaji 44 iliyopatikana kupitia kura ya mtandaoni. Wachezaji 11 walichujwa na kusalia na 33 watakaowania kuwa katika 11-bora wa KEFWA. Mfungaji bora wa 2020-2021 Tereza Engesha kutoka Vihiga Queens yuko kwenye orodha ya wanaopigiwa upatu kuibuka mshambuliaji bora, ingawa mwenzake Jentrix Shikangwa aliyeng’ara nje ya ligi katika michuano ya kufuzu kushiriki makala ya kwanza ya Klabu Bingwa Afrika, hakujumishwa popote.

Washindi watapata fursa ya kutangamana na washauri kutoka ndani na nje ya michezo. Katibu wa KEFWA, Jerry Santo alisema Alhamisi kuwa kupitia miradi ya chama hicho kama Bridge The Gap, Mind The Gap na Raising Our Game, wachezaji watapata kukubali taaluma nyingine nje ya uchezaji wa soka kama njia ya kujiandaa kwa maisha baada ya uchezaji.

“Hafla hii si ya kutuza tu wachezaji, bali jukwaa la kujifunza kutoka kwa wanawake wengine waliofaulu maishani na wenye ushawishi mkubwa kutoka sekta ya biashara na mashirika mbalimbali. Tunatumai kuwa washauri hao na mifano bora watawaelekeza katika uanasoka pamoja na taaluma nyingine,” aliongeza Santo.

Hii hapa orodha ya wawaniaji 33:

Makipa

Judith Osimbo (Gaspo Women)

Monica Karambu (Thika Queens)

Monica Chebet (Wadadia Women)

Mabeki wa pembeni kushoto

Enez Mango (Vihiga Queens)

Wincate Kinyua (Thika Queens)

Lavender Akeyo (Zetech Sparks)

Mabeki wa pembeni kulia

Vivian Nasaka (Vihiga Queens)

Miriam Chelegat (Wadadia Women)

Joan Naututu (Ulinzi Starlets)

Mabeki wa kati pembeni kushoto

Phoebe Aketch (Vihiga Queens)

Juliet Andipo (Kayole Starlets)

LucyAkoth (Mathare Women)

Mabeki wa kati pembeni kulia

Dorcas Sikobe (Thika Queens)

Miriam Asangira (Gaspo Women Fc)

Phelistas Kadari (Vihiga Queens)

Kiungo wa kati mkabaji

Mercyline Wayodi (Kisumu All Starlets)

Sheril Angachi (Gaspo Women)

Joan Nabirye (Vihiga Queens)

Kiungo mshambuliaji wa pembeni kulia

Rebecca Okwaro (Nakuru Queens)

Cindy Ngaira (Wadadia Women)

Rael Kamanda (Makolanders)

Kiungo mshambuliaji wa pembeni kushoto

Martha Karani (Trans-Nzoia Falcons)

Lydia Waganda (Thika Queens)

Lydia Akoth (Zetech Sparks)

Mshambuliaji wa pembeni kushoto

Neddy Okoth (Ulinzi Starlets)

Rachael Muema (Thika Queens)

Mercy Airo (Gaspo Women)

Mshambuliaji wa pembeni kulia

Jereko Mwanahalima Dogo (Thika Queens)

Ruth Chebungei (Wadadia Women)

Elizabeth Mutukiza (Gaspo Women)

Mshambuliaji wa kati

Rasoa Sylia (Ulinzi Starlets)

Tereza Engesha (Vihiga Queens)

Christine Ngoizi (Kayole Starlets)

You can share this post!

20 kuwania taji la Guru Nanak Rally msimu ukifika kilele

Kisumu All Stars, Zoo Kericho ugani wikendi

T L