Michezo

Kenya ingali mbali kufikia dhahabu kwenye voliboli Afrika

March 16th, 2018 1 min read

Na GEOFFREY ANENE

KLABU za Pipeline na Prisons zilishindwa kutimiza ahadi ya kushindia Kenya medali ya dhahabu kwenye mashindano ya voliboli ya Klabu Bingwa Afrika ya Wanawake yaliyokamilika nchini Misri, Alhamisi.

Mabingwa mara tano Pipeline, ambao mara ya mwisho walikuwa malkia wa Afrika ni mwaka 2005, waliridhika na nishani ya shaba baada ya kuzima mabingwa mara tano Prisons 3-2 (23-25, 25-21, 29-27, 15-11).

Prisons inasalia klabu ya mwisho kutoka Kenya kunyakua ubingwa wa Afrika mwaka 2013. Wanamagereza hawa walivuna mwaka 2008, 2010, 2011, 2012 na 2013 na kuambulia medali ya fedha mwaka 2014 na 2015 na shaba mwaka 2017.

Pipeline walitawazwa mabingwa wa Afrika mwaka 1998, 2001, 2002, 2004 na 2005 na kujishindia fedha mwaka 2003, 2007, 2010, 2011, 2012 na 2015. Walishinda medali ya shaba mwaka 2014, 2016 na 2018.

Wenyeji Al Ahly walinyakua taji lao la tisa la Afrika baada ya kulipua mabingwa wa mwaka 2017 Carthage 3-0.

JEDWALI (mwaka 2018):

1.Al Ahly (Misri)

2.Carthage (Tunisia)

3.Pipeline (Kenya)

4.Prisons (Kenya)

5.Revenue (Rwanda)

6.Bafia (Cameroon)

7.Shams (Misri)

8.Customs (Nigeria)

9.Nkumba (Uganda)

10.INJS (Cameroon)

11.Vision (Uganda)

12.Chlef (Algeria)

13.Nyong (Cameroon)

14.Harare City (Zimbabwe)

15.FAP (Cameroon)

16.Asec Mimosas (Ivory Coast)

17.DGSP (Congo Brazzaville)

18.Douanes (Burundi)

19.BDF (Botswana)