Kenya kuadhimisha Siku ya Utamaduni

Kenya kuadhimisha Siku ya Utamaduni

Na WINNIE ONYANDO

SERIKALI imetangaza Jumatatu kuwa siku ya mapumziko, Kenya ikiadhimisha kwa mara ya kwanza Siku ya Utamaduni Oktoba 10, 2021.

Waziri wa Usalama, Dkt Fred Matiang’i alisema kuwa Jumatatu itakuwa siku ya mapumziko kwa sababu siku ya Utamaduni inayostahili kusherehekewa Oktoba 10, ni Jumapili.

“Hii ndio siku ya kwanza tunasherehekea siku ya Utamaduni nchini. Tunafaa kuitumia siku hiyo kusisitiza hitaji la raia wote kutambua na kusherehekea utamaduni huu tajiri wa Kenya kwa njia ambayo inakuza umoja, mshikamano wa kitaifa na maendeleo ya kiuchumi nchini Kenya,” akasema Dkt Matiangi.

Awali, siku hii ilikuwa ikiadhimishwa kama Moi Dei kwa heshima ya aliyekuwa rais wa pili wa Kenya, Daniel arap Moi.

You can share this post!

Hatima ya uchaguzi mdogo kujulikana leo

Amerika yatoa ahadi kusaidia Joho kufufua uchumi wa kaunti...