Kenya kukaribisha mataifa saba Kombe la Dunia raga ya Under-20 Julai

Kenya kukaribisha mataifa saba Kombe la Dunia raga ya Under-20 Julai

Na GEOFFREY ANENE

KENYA imeteuliwa kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia la raga ya daraja la pili la chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20.

Kombe hilo, ambalo timu ya taifa ya Kenya almaarufu Chipu ilishiriki mwaka 2009 (Nairobi) na 2019 (Brazil), litafanyika Julai 15-30 mjini Nairobi ambapo bingwa ataingia daraja la kwanza.

Mashindano ya daraja la kwanza la U20 yataandaliwa nchini Afrika Kusini mnamo Juni 24 hadi Julai 14.

Makombe haya yanarejea baada ya makala ya 2020, 2021 na 2022 kufutiliwa mbali kwa sababu ya janga la virusi vya corona.

Daraja la kwanza litahusisha Argentina, Australia, Uingereza, Fiji, Ufaransa, Georgia, Ireland, Italia, Japan, New Zealand, Afrika Kusini na Wales. Daraja la pili litajumuisha Scotland (ilitemwa kutoka daraja la kwanza mwaka 2019), Kenya (wenyeji), Hong Kong (Asia), Samoa (Oceania), Uhispania (Ulaya), Uruguay (Amerika ya Kusini) na timu moja kutoka Amerika ya Kaskazini na Afrika zitakazofuzu kupitia mashindano ya kanda hizo.

Scotland, Uruguay, Canada ama Amerika, na Afrika 2 wako Kundi A nao Uhispania, Samoa, Kenya na Hong Kong watakabiliana katika Kundi B.

Rais wa Shirikisho la Raga Duniani, Sir Bill Beaumont alisema wamefurahia kuzindua wenyeji wawili wa makombe hayo ya 2023. Afrika Kusini na Kenya zitatupa majukwaa sawa ya kurejea kwa mashindano yetu ya U20 yanayochangia pakubwa katika kukuza talanta changa katika mashirikisho yetu,” alisema.

  • Tags

You can share this post!

Arsenal ina kibarua kingine leo Ijumaa

KIKOLEZO: Vita vya MCSK, KECOBO vyafikia patamu

T L