NA KALUME KAZUNGU
VINARA wa Muungano wa Kenya Kwanza, wamependekeza gavana wa zamani wa Lamu, Bw Issa Timamy (pichani) apeperushe bendera ya muungano huo katika uchaguzi wa ugavana Lamu.
Bw Timamy anatarajiwa kupigania kiti hicho alichopoteza 2017, kupitia Chama cha Amani National Congress (ANC).
Katika uchaguzi uliopita, alishindwa na Gavana Fahim Twaha, wa Jubilee.
Aliungwa mkono katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na kinara wa Ford Kenya, Bw Moses Wetang’ula, Seneta wa Tharaka Nithi, Bw Kithure Kindiki, mwenzake wa Lamu, Bw Anwar Loitiptip miongoni mwa wengine.