Kenya Police warapua Vihiga kuingia FKF-PL

Kenya Police warapua Vihiga kuingia FKF-PL

Na JOHN ASHIHUNDU

TIMU ya Kenya Police imeingia kwenye Ligi Kuu ya Kenya (FKF-PL).

Kikosi hicho kinachonolewa na John Bobby Ogolla kilipata nafasi hiyo baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Vihiga United katika mechi ya marudiano.

Timu hizo zilikuwa zimefungana 1-1 katika mechi ya mkondo wa kwanza iliyochezewa Mumias Complex, wiki iliyopita.

Kutokana na matokeo hayo, Vihiga imeshuka ngazi hadi Supa Ligi baada ya juhudi zao kuvurugwa na bao la Kelvin Kinanga dakika ya 33.

Kocha Ogolla alisema vijana wake walicheza kulingana na alivyopanga, huku akiisifu safu yake ya ulinzi kwa kukaa ngumu hadi dakika ya mwisho katika mechi hiyo iliyochezewa ugani Utalii.

You can share this post!

Amani: Kalonzo kutuzwa leo Dubai

TAHARIRI: Vijana wasikubali siasa za vurugu