Habari Mseto

Kenya Re yapungukiwa na faida

August 25th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Kampuni ya Kenya Reinsurance Corporation (Kenya Re) imepungukiwa na faida kwa asilimia 24.19 katika nusu ya kwanza ya 2018.

Hiyo ilitokana na kupungukiwa na mapato kutokana na kupungua kwa malipo ya bima.

Faida ilikuwa Sh1.22 bilioni katika muda huo ikilinganishwa na Sh1.62 bilioni ilizopata kipindi hicho 2017.

Malipo ya bima yaliipa kampuni hiyo asilimia ya 10.12 ya mapato yake ya Sh6.37 bilioni wakati wa kipindi hicho.

Vile vile, biashara yake ya kimataifa, ambayo huchangia asilimia 40 ya mapato yake iliathiriwa vibaya.

Ilipata hasara Ghana, Nigeria, India, Ethiopa na Nepal. Kenya Re hutoa bima kwa kampuni 160 katika mataifa 45 ya Afrika, Mashariki ya Kati na Asia.