Kenya Simbas wararua Uganda bila huruma Kombe la Afrika la kuingia Kombe la Dunia

Kenya Simbas wararua Uganda bila huruma Kombe la Afrika la kuingia Kombe la Dunia

Na GEOFFREY ANENE

KENYA Simbas wameanza kampeni ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia 2023 kwa kurarua Uganda Cranes kwenye robo-fainali ya Kombe la Afrika nchini Ufaransa, leo Jumamosi.

Simbas, ambayo haijawahi kuingia Kombe la Dunia katika historia yake, itamenyana na katika nusu-fainali na mshindi kati ya Senegal na Algeria. Hapo Jumamosi, Simbas iliongoza dakika 40 za kwanza 28-0 kupitia miguso minne kutoka kwa John Okoth Thomas Okeyo Samuel Asati na Bethwel Anami iliyoandamana na mikwaju ya Darwin Mukidza katika mechi ya kusisimua.

Vijana wa kocha Paul Odera, ambao wakati mmoja katika kipindi cha kwanza walinufaika na Pius Ogena kulishwa kadi ya njano, walirejea kwa kishindo kutoka mapumzikoni walipoongeza miguso miwili ya haraka kupitia kwa Okoth na nguvu-mpya Teddy Akala ambayo Mukidza na mzawa wa Fiji Jone Kubu waliongeza mkwaju mtawalia.

Hata hivyo, Jacob Ochen alifungia Waganda mguso wa kufutia machozi ulioandamana na mkwaju kutoka kwa Philip Wokorach na kupunguza uongozi wa Simbas hadi 42-7.

Nusu-fainali nyingine itakutanisha mabingwa watetezi Namibia waliorarua Burkina Faso 71-5, na Zimbabwe iliyopepeta Ivory Coast 38-11, Julai 1. Mshindi wa Afrika mnamo Julai 10 atajikatia tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia 2023 nchini Ufaransa.

  • Tags

You can share this post!

Cherotich, Wanyonyi wakata tiketi ya Riadha za Dunia U20...

Aliyekuwa kipa nguli wa Rangers na timu ya taifa ya...

T L