Habari Mseto

Kenya yakataa mkopo wa Sh150 bilioni

August 15th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Kenya haitatia sahihi mkopo wa bima kutoka kwa Hazina ya Fedha ya Kimataifa (IMF) wa Sh150 bilioni.

Mkopo huo umetolewa kukinga taifa hili kutokana na mtingisiko wa kutoka nje wa uchumi.

Lakini IMF iliweka masharti magumu ikiwemo ni pamoja na kuondoa viwango vya mwisho vya riba, na ndio maana serikali imekataa kutia sahihi mkopo huo.

Ripoti hii ni kwa mujibu wa mshauri katika Afisi ya Rais Mbui Wagacha, ambaye pia ni mwanauchumi.

Jumanne, alisema mapendekezo hayo ya IMF kama ambayo yanalenga sera za uchumi za Kenya hayaambatani na ukweli uliopo nchini.

Kauli yake imeonekana kuunga mkono msimami wa Benki Kuu ya Kenya (CBK) na huenda ukaathiri uhusiano kati ya Kenya na IMF.