Kenya yamaliza mkiani voliboli ya kinadada Olimpiki

Kenya yamaliza mkiani voliboli ya kinadada Olimpiki

Na GEOFFREY ANENE

MALKIA Strikers wamekamilisha kampeni yao ya Olimpiki 2020 katika nafasi ya mwisho (12) baada ya kupoteza michuano yake yote ya Kundi A nchini Japan.

Kenya, ambayo iliongozwa kwenye Olimpiki na kocha Mbrazil Luizomar de Moura akisaidiwa na Mkenya Paul Bitok na Mbrazil Jefferson Arost, imelimwa na Brazil kwa seti 3-0 za alama 25-10, 25-16, 25-8 katika ukumbi wa Ariake jijini Tokyo mnamo Agosti 2.

Sharon Chepchumba aliibuka mfungaji bora wa Kenya katika mechi hiyo ambayo ilidumu saa moja na dakika nne. Mbrazil Ana Carolina da Silva alifunga alama nyingi katika mechi hiyo (12).

Malkia Strikers ilikaribishwa kwenye Olimpiki za Tokyo kwa kichapo cha 3-0 (25-15, 25-11, 25-23).

Kisha, mabingwa hao wa zamani wa Afrika, ambao hawakufuzu kushiriki makala ya 2008 (Beijing, Uchina), 2012 (London, Uingereza) na 2016 (Rio de Janeiro, Brazil), walipoteza 3-0 dhidi ya Korea Kusini (25-14, 25-22, 26-24), Serbia (25-21, 25-11, 25-20) na Dominican (25-19, 25-18, 25-10).

Uchina imekamilisha katika nafasi ya tisa baada ya kushinda michuano miwili katika Kundi B. Wenyeji Japan wamamaliza katika nafasi ya 10 kutokana na ushindi dhidi ya Kenya. Argentina imeridhika katika nafasi ya 11, mbele ya Kenya kwa tofauti ya ubora wa seti, ingawa pia haikushinda mchuano wowote katika kundi la pili.

Brazil (alama 14), Serbia (12), Korea Kusini (saba) na Dominican (nane) walijikatia tiketi za kushiriki robo-fainali kutoka kundi la kwanza nao Amerika (10), Italia (10), Uturuki (9) na Urusi (9) wakafuzu kutoka kundi la pili.

  • Tags

You can share this post!

Obiri aridhika na medali ya fedha tena Olimpiki

Mvutano mitandaoni baada ya Raila kutumia gari la serikali