Kenya yapigiwa debe kuandaa Riadha za 2025

Kenya yapigiwa debe kuandaa Riadha za 2025

Na AYUMBA AYODI

KENYA imepata uungwaji mkono kutoka kwa nyota Mwingereza Paula Radcliffe katika juhudi zake za kuwa mwenyeji wa Riadha za Dunia 2025.

Mshikilizi huyo wa zamani wa rekodi ya dunia mbio za kilomita 42 za kinadada yuko Kenya kwa shughuli za kusaidia wasiojiweza. Anasema kuwa Kenya imeonyesha ina uwezo wa kuandaa mashindano makubwa ya riadha baada ya kufaulu uenyeji wa Riadha za Dunia za chipukizi wasiozidi umri wa miaka 18 mwaka 2017 na walio chini ya umri wa miaka 20 mwezi Agosti 2021.

Bingwa huyo wa zamani wa dunia wa Nusu-Marathon na Marathon alisema pia mafanikio katika kuandaa duru ya Riadha za Continental Tour ya Kip Keino ni ishara kuwa Kenya ina uwezo.“Riadha za Dunia za Under-18 hazikuwa na matatizo na pia nilikuwa hapa kushuhudia ya Under-20,” alisema na kuongeza kuwa Bara Afrika limekuwa na wanariadha wengi, lakini halijawakilishwa vyema katika idadi ya mashindano.

Rais wa Shirikisho la Riadha Duniani Sebastian Coe aliwahi kuelezea hamu yake ya kuona Afrika ikiandaa mashindano hayo 2025 ambayo Kenya imeomba. Wapinzani wa Kenya ni Poland, Singapore na Japan.

You can share this post!

Tusker FC, Wazito na Police zazoa ushindi

Jasiri wa Kenya watamba miereka ya Tong-Il Moo-Do

T L