Habari

Kenya yathibitisha kisa cha kwanza cha virusi vya Corona

March 13th, 2020 1 min read

Na MWANDISHI WETU

KENYA imethibitisha kisa cha kwanza cha virusi vya Corona kwa mwanamke aliyetua jijini Nairobi akitoka nchini Amerika.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema Ijumaa kwamba kisa hicho kiligundulika Alhamisi, lakini akasema mgonjwa anaendelea vizuri.