Habari

Kenya yathibitisha visa 30 vipya vya maambukizi ya Covid-19 idadi jumla ikifika 465

May 3rd, 2020 1 min read

Na MWANDISHI WETU

KUFIKIA leo Jumapili Kenya ina visa 30 vipya vya maambukizi ya Covid-19 ambapo Mombasa ina visa 19, Nairobi (8), Bungoma (2) na Kitui (1).

Waziri Msaidizi katika Wizara ya Afya Dkt Rashid Aman amesema taifa hili sasa limerekodi idadi jumla ya visa 465 tangu kisa cha kwanza kitangazwe Machi 13, 2020.

Wahanga wa maradhi hayo nchini wamefika watu 24 baada ya watu wawili zaidi kufariki mjini Mombasa.

Nayo idadi ya waliopona imefika watu 167 baada ya wizara kuruhusu watu wengine 15 kuondoka hospitalini.

Akitoa ripoti ya hali ya taifa ya kila siku kuhusu Covid-19, Dkt Aman amesema masharti magumu zaidi yamewekwa na serikali.

“Maafisa wa polisi wanaenda kutenga maeneo maalum ya kuwaweka karantini wanaokiuka kafyu na maagizo muhimu ya kujikinga kuepuka maambuklizi ya Covid-19,” amesema.