Habari Mseto

Kesi ya Karua dhidi ya Waiguru kusikizwa na majaji wapya

August 1st, 2018 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA ya rufaa Jumanne iliamuru kesi ya kupinga ushindi wa Gavana Anne Waiguru kuwa Gavana wa Kirinyaga isikizwe na majaji wapya.

Waziri wa zamani wa masuala ya katiba Bi Martha Karua aliwasilisha ombi katika mahakama ya rufaa akisema “ hataki kesi yake isikizwe na majaji walio katika mahakama ya rufaa ya Nyeri.”

Alisema majaji hao wameonyesha upendeleo na anahofia kwamba hatapata haki katika kesi aliyomshtaki Bi Waiguru.”

Majaji Asike Makhandia , Daniel Musinga na Kairu Gatembu walisema malalamishi ya Bi Karua yalikuwa na msingi.

Majaji hao waliamuru majaji wengine wateuliwa na rais wa mahakama hiyo Jaji William Ouko.

Bi Karua aliwasilisha alipinga ushindi wa Bi Waiguru akisema hakushinda kiti hicho kwa njia halali.