Habari Mseto

Kesi ya Kitany na Linturi yaanika mengi

August 21st, 2019 2 min read

Na MARY WANGARI

[email protected]

KESI ya talaka kati ya Seneta wa Meru Mithika Linturi na anayedai kuwa ni mkewe, Bi Maryanne Kitany, imeibua hisia kali ikiibua siri kuu ikiwemo jinsi mswada uliolenga kumtimua Gavana Anne Mumbi, kuhusiana na sakata ya Sh791 milioni, ulivyosambaratishwa.

Akitoa ushahidi Jumanne, Agosti 20, katika kesi hiyo ambayo imegonga vichwa vya vyombo vya habari nchini, Bi Kitany, aliyekuwa mkuu wa wafanyakazi katika afisi ya Naibu Rais William Ruto, aliieleza mahakama jinsi alivyoweza kumshawishi Seneta Linturi kufutilia mbali juhudi za kumng’atua mamlakani Gavana wa Kirinyaga, kuhusiana na sakata ya ufujaji wa Sh791 milioni za Shirika la Huduma ya Vijana kwa Taifa (NYS).

Kulingana na Bi Kitany, Seneta huyo wa Meru alikuwa pamoja naye mjini Naivaisha kwa ziara ya mapenzi, badala ya kuhudhuria kikao cha bunge alipotakiwa kuwasilisha mswada dhidi ya Gavana Mumbi.

“Linturi alikuwa nami katika hoteli ya Sopa Lodges badala ya kuwa Bungeni kuwasilisha mswada wa kumtimua Waiguru,” alisema Kitany.

Akaongeza: “Alikuwa tayari ameuteka moyo wangu.”

Bi Kitany alimfichulia Jaji Peter Ngare katika mahakama ya Milimani jinsi Naibu Rais alivyojaribu mnamo 2014 kumrai Linturi, aliyekua amejitwika jukumu la kuwasilisha mswada bungeni dhidi ya Mumbi, kuutupilia mbali kwa kuwa ungeathiri vibaya chama cha Jubilee.

Hata hivyo, kulingana na Keitany, juhudi za Ruto ziligonga mwamba huku Linturi akishikilia msimamo wake wa kuwasilisha mswada huo bungeni hadi upitishwe, hali iliyomfanya naibu rais kumtaka Keitany kuingilia kati.

Seneta Linturi aliyekuwa wakati huo amechaguliwa tena kama mbunge wa Igembe Kusini, aliibua ghadhabu miongoni mwa wanasiasa wenzake, baada ya kutoweka siku ya kutajwa kwa mswada aliowasilisha na kuusababisha kutupiliwa mbali.

Akijitetea kwa kukosa kufika bungeni, Linturi alieleza vyombo vya habari Juni 2014, kwamba hakutaka kwenda kinyume na Rais Uhuru Kenyatta.

“Tumetoka mbali na Rais na singependa mswada huo uje kati yetu, Hakuna anayetaka kubembelezwa na Rais, si vyema hasa katika suala linalohusu maslahi ya taifa,” alisema.

Bi Kitany, aliyewasilisha kesi ya kumtaliki Linturi mnamo 2018 akitaja uasherati, dhuluma, na kuwa na ndoa mbili, pia alifichua jinsi seneta huyo alivyohamia nyumbani kwake Kileleshwa.

“Tulikuwa tukiishi na Linturi nyumbani kwangu Kileleshwa. Alihamia kwangu,” alisema.

Kuhusu madai ya Linturi kwamba hakuwahi kumwoa, Kitany alisema waliishi kama mke na mume baada ya seneta huyo kumtambulisha rasmi kwa wazazi wake kama mkewe.

“Nilitambulishwa rasmi kwa wazazi wa Linturi kama mkewe. Tulijadili kuhusu kuifanya ndoa yetu kuwa rasmi 2016 na akasema alitaka kwenda kwetu papo hapo. Ni yeye (Linturi) aliyeniposa. Nilikubali na watu wake wakaja kwetu na wakachagua likizo ya Pasaka,” alifichua.