Habari Mseto

Kesi ya Mwilu yavutia wanahabari kutoka kona zote za dunia

August 30th, 2018 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

WANAHABARI wa humu nchini na kimataifa walifurika mahakama ya Milimani Nairobi Jumatano kufuata kesi aliyoshtakiwa naibu wa Jaji Mkuu (DCJ) Philomena Mwilu.

Polisi wanaoshika doria mahakama walikabiliwa na wakati mgumu kuwazuia wanahabari wasimkaribie hakimu mkuu Lawrenze Mugambi aliyekuwa anasikiza kesi dhidi ya jaji huyo aliye pia naibu wa Rais wa Mahakama ya Juu.

Wanahabari wamekuwa na bidi ya mchwa wakifuatilia kesi za ufisadi dhidi ya washukiwa ambao wamekuwa wakifikishwa mahakamani siku za hivi punde.

Baadhi ya mawakili walishambulia vyombo vya habari kwa kuripoti kwamba Jaji Mwilu ameporomoka.

Hata hivyo mahakama haikusema chochote kuhusu madai kuwa vyombo vya habari vimejadili masuala ya kesi hiyo kwa kina.

Kesi dhidi ya Jaji Mwilu itatajwa Ijumaa.