Kesi ya ufisadi ya Sh7.4Bn dhidi ya Mbunge Rigathi Gachagua kuskizwa Septemba 2022

Kesi ya ufisadi ya Sh7.4Bn dhidi ya Mbunge Rigathi Gachagua kuskizwa Septemba 2022

Na RICHARD MUNGUTI

KESI ya ufisadi inayomkabili Mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua ya ufujaji wa zaidi ya Sh7.4bilioni itaanzaz kusikizwa baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti 2022 katika mahakama ya Milimani Nairobi

Hakimu mwandamizi Rose Makungu aliamuru kesi hiyo isikizwe Septemba 5 2022 baada ya kuelezwa upande wa mashtaka haujamkabidhi Gachagua nakala ushahidi. Bi Makungu alisema kati ya Janauri na Julai 2022 mahakama ya kuamua kesi za ufisadi imeorodhesha kesi nyingine zikiwamo zile za kashfa ya shirika la huduma ya vijana kwa taifa NYS.

“Kati ya Januari na Julai mwaka ujao hii mahakama imeorodhesha nyingine za ufisadi.Itabidi kesi hii dhidi ya Gachagua itengewe siku miezi ya Septemba , Oktoba na Novemba 2022,”alisema Bi Makungu. Pia hakimu alisema mshtakiwa hajaklabidhiwa nakala za mashahidi.

Mawakili Gibson Kimani na Kioko Kilukumi wanaomtetea Bw Gachagua anayeshtakiwa pamoja na watu wengine tisa walisema pia wanahusika katika kesi nyingine zitakazoanza kusikizwa kati ya Januari na Agosti 2022. Mawakili wa Gachagua walilamika kuwa miezi saba imepita tangu mbunge huyo ashtakiwe na upande wa mashtaka haujamkabidhi nakala za mashahidi.

“Upande wa mashtaka ulisema uomeorodhesha mashahidi 45. Tunatazamia nakala za mashahidi 45. Hatujapokea ushahidi huu,” Bw Kimani alieleza mahakama. Wakili huyo alisema walipokea nakala chache jana asubuhi na “wanahitaji muda kujiandaa.”

Upande wa mashtaka ulithibitisha kwamba haujamkabidhi Gachagua ushahidi wote. Hata hivyo kiongozi wa mashtaka aliomba mahakama itenge siku kati ya 10-14 katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Septemba ili wakamilishe kusikiza kesi hiyo.

Mahakama iliombwa itenge siku tano katika kila mwezi kuanzia Septemba 5,2022. Bw Gachagua alikanusha mashtaka ya ufisadi wa Sh7.4bilioni. Upande wa mashtaka unadai mbunge huyo alipokea zaidi ya Sh7bilioni akijua zimepatikana kwa njia isiyo halali kati ya 2013 na 2020.

Inadaiwa Bw Gachagua kupitia kwa kampuni zake alijinufaisha na pesa za umma. Bw Gachagua amshtakiwa pamoja na meneja wa hazina ya CDF Mathira William Mwangi Wahome, Ann Nduta Ruo, Jullianne Jahenda Makaa na Samuel Murimi Ireri, Grace Wambui Kariuki, Lawrence Kimaru, Irene Wambui Ndigiriri, David Reuben, Nyangi Nguru na Rapid Medical Supplies Ltd.

Mbunge huyo amekabiliwa na mashtaka ya kula njama za kuilaghai serikali na ulanguzi wa pesa. Bw Gachagua yuko nje kwa dhamana ya Sh12milioni.

You can share this post!

Pigo West Ham beki tegemeo Kurt Zouma akiingia mkekani

Beki wa zamani wa Liverpool, Maxi Rodriguez, astaafu soka

T L