KFS yapinga kesi ya kuzima Mpesa Likoni

KFS yapinga kesi ya kuzima Mpesa Likoni

Na PHILIP MUYANGA

SHIRIKA la Huduma za Feri (KFS) limeomba mahakama itupilie mbali kesi inayopinga utumizi wa mfumo wa Mpesa kulipia ada za kuvuka feri Likoni, Kaunti ya Mombasa.

Kulingana na KFS, mfumo huo ulinuiwa kutekeleza mwongozo wa serikali uliohitaji watu waepuke matumizi ya sarafu ili kuepusha ueneaji wa virusi vya corona.

Katika utetezi wake katika kesi iliyowasilishwa mahakamani na shirika la kutetea haki za binadamu la Muslims for Human Rights (Muhuri), KFS imesema Muhuri inapoteza muda wa mahakama kwa kuwa madai yake hayana msingi.

Kupitia hati ya kiapo ya Mkurugenzi Mkuu wa KFS, Bakari Hamisi Gowa, KFS ilidai hakuna mtu yeyote ambaye hukatazwa kuvuka feri kama hawezi kulipa ada kupitia simu na ana pesa taslimu.

Alieleza kuwa, kuna maajenti ambao wameruhusiwa kupokea pesa taslimu kutoka kwa wasafiri ambao hawana uwezo wa kulipa kwa simu, na kuna mpango mahsusi ambao huhakikisha pesa zinazokusanywa zinafikia shirika hilo.

You can share this post!

BBI: Serikali yaandaa rufaa ya uamuzi

Covid: Magavana zaidi katika hatari ya kuadhibiwa