Kiangazi chaangamiza mifugo 2.5 milioni

Kiangazi chaangamiza mifugo 2.5 milioni

NA WINNIE ATIENO

KIANGAZI kinachoshuhudiwa nchini kimeangamiza zaidi ya mifugo 2.5 milioni huku serikali ikitafuta njia ya kunusuru wafugaji dhidi ya jinamizi hilo ambalo linaendelea kuwasababishia hasara.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Mifugo Bw Harry Kimtai alisema serikali inashughulikia suala hilo kupitia uuzaji wa mifugo hiyo nje ya nchi ili kuzuia hasara zaidi katika maeneo athirika.

Bw Kimutai alisema takriban mifugo 2.5 wameaga duania kutokana na kiangazi hicho huku wengine wakisalia katika hatari kufuatia kiangazi nchini.

“Mifugo iliyosalia haiko katika hali nzuri. Uzito umepungua kwa sababu ya ukosefu wa malisho na kutembea muda mrefu kutafuta maji. Tuna ng’ombe lakini bei yao sokoni iko chini sana kwa sababu afya yao imedhohofika,” alisema Bw Kimtai.

Licha ya hayo, alieleza kuwa serikali ipo tayari kutafuta njia mbadala ya kuwasaidia wafugaji wa humu nchini.

Kupitia tume ya kusimamia nyama nchini (KMC), wafugaji hao wanaweza kuuza mifugo yao kabla ya kupata hasara. Bw Kimutai, aliwataka wafugaji kuuza ngombe wao kuelekea Gulf baada ya Kenya kuingia katika makubaliano ya kuuza mifugo hiyo katika nchi ya Oman.

“Tumeungana na nchi za uarabuni ili waweze kununua mifugo wetu. Tunawauza ng’ombe wetu Oman kupunguza idadi ya mifugo tulionao nchini haswa sasa tunapokabiliwa na kiangazi,” alisema Bw Kimtai.

Akizungumza katika maonyesho ya kisayansi yalioandaliwa na shirika la uzalishaji wa mifugo nchini (APSK), katibu huyo alieleza kuwa Kenya iko katika hali ngumu kwa kukosa mvua kwa takriban misimu minnne. Hali hiyo alieleza kuwa ni mbaya zaidi katika sehemu ya Kaskazini mashariki mwa nchi ambako kuna mifugo wengi sana.

“Kaskazini mashariki mwa Kenya ndiko kunategemewa kwa uzalishaji wowote wa kimifugo. Iwapo hatutawekeza katika kilimo kinachojali hali ya hewa, kilimo cha mifugo kitathirika. Ndiposa leo tuna mkutano huu na wakulima ili tuwaeleze kuhusu masula haya,” alisema Bw Kimutai.

Katibu huyo alieleza kuwa maonyesho hayo ambayo mada yake ni mfumo wa chakula endelevu , na uzalishaji wa mifugo unaojali hali ya hewa, utaisaidia serikali kuandaa sera zinazohusu sekta ya uzalishaji wa mifugo.

“Tunataka kutafuta jinsi tutakavyoendeleza kilimp cha mifugo licha ya mabadiliko ya hali ya hewa. Wataalamu wote katika sekta ya mifugo wanaojihusisha na lishe bora na ufundi wapo hapa kutafuta mikakati mwafaka ya ufugaji,” Bw Kimtai.

Alieleza kuwa wataalamu hao wataisaidia wizara katika utafiti na kupiga jeki uzalishaji wa mifugo.

Bw Kimutai alieleza kuwa wafugaji watapata mafunzo ya jinsi ya kuendeleza kilimo cha mifugo licha ya sehemu tofauti ya wanakotoka.

Aliwasihi wakulima wa eneo la mlimani na wale wa kaskazini mwa bonde la ufa ambao wamekuwa wakifaidi na mvua ya kutosha, kupanda malisho ya mifugo ambayo inaweza kuuzwa kwa wafugaji kuendeleza kilimo cha ng’ombe wanaofugwa kwa sababu ya nyama.

You can share this post!

NDIVYO SIVYO: Matumizi uchwara ya kihusishi ‘miongoni...

Kaptich, Kosgey wavizia mataji ya Frankfurt Marathon

T L