Kiangazi: Wakulima hatarini kupoteza mimea

Kiangazi: Wakulima hatarini kupoteza mimea

Na DAVID MUCHUI

WAKULIMA katika Kaunti ya Meru wako hatarini kupata hasara, baada ya mazao yao kunyauka kutokana na hali ya kiangazi inayoendelea.

Hali hiyo pia imechangiwa na mvua chache inayoendelea kunyesha katika eneo hilo mwezi huu. Wakulima walioathiriwa ni wale walio katika maeneo ya Tigania Magharibi, Tigania Mashariki, Igembe ya Kati, Igembe Kaskazini na Igembe Kusini.

Wakulima hao hutegemea kilimo kujiendeleza kimaisha. Kutokana na hali hiyo, sasa wanaitaka serikali kuingilia kati ili kuwasaidia. Katika baadhi ya sehemu za eneo la Igembe Kaskazini, hali hiyo imechangia zao la miraa. Zao hilo huwa kitegauchumi kwa wakazi.

Kulingana na Shirika la Utabiri wa Hewa Kenya (KMD), hali hiyo ni dalili za msimu wa ‘La Nina’, ambao huwa ni mvua chache kuliko ilivyotarajiwa. Bw Martin Muriithi, ambaye ni mkazi wa Rei, Tigania Magharibi, alisema ni mvua chache sana ambayo imenyesha katika eneo hilo kwa muda mrefu.

“Mvua hiyo ilinyesha kwa siku moja pekee. Mbegu tulizokuwa tumepanda zilimea. Mimea hiyo sasa imeanza kunyauka kutokana na ukosefu wa mvua. Matumaini yetu yameanza kudidimia ikizingatiwa tulitumia fedha nyingi kuzinunua,” akasema Bw Muriithi.

You can share this post!

Serikali kuunda idara ya kufuatilia matumizi ya pesa

Wafungwa wataka haki sawa na raia huru 2022

T L