Kibarua kigumu cha Okutoyi robo-fainali ya tenisi ya Monastir

Kibarua kigumu cha Okutoyi robo-fainali ya tenisi ya Monastir

Na GEOFFREY ANENE

MKENYA Angella Okutoyi na mchezaji mwenza Akanksha Nitture wanatarajiwa kupata kibarua kigumu katika robo-fainali ya shindano la tenisi la akina dada la W15 Monastir nchini Tunisia kuanzia saa nane na nusu Alhamisi.

Watakutana na Nina Radovanovic (Ufaransa) na Xinxin Yao (Uchina) ambao wanaorodheshwa wa pili katika mashindano haya.

Okutoyi na Nitture, ambaye ni raia wa India, walijikatia tiketi ya kushiriki robo-fainali baada ya kuwabandua Zuzanna (Poland) na Magdalena Stoilkovska (North Macedonia) kwa seti 2-1 za 6-3, 1-6, 10-5 Jumatano. Mechi hiyo ilichukua saa moja na dakika 21 nao Radovanovic na Yao walilima Ferdaous Bahri (Tunisia) na Margaux Komano (Ufaransa) 6-2, 6-3.

Okutoyi, ambaye alishinda taji la chipukizi la Wimbledon mwezi Julai, alibanduliwa na Shrivalli Bhamidipaty kutoka India katika raundi ya kwanza ya kitengo cha mchezaji mmoja kila upande mnamo Agosti 2.

Bingwa huyo wa Kenya Open 2018 na Afrika kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 18 mwaka 2021 alitoa Bhamidipaty kijasho kabla ya kusalimu amri kwa seti mbili kavu za 7-6(5), 7-5 katika klabu ya tenisi ya Monastir.

  • Tags

You can share this post!

VYAMA: Chama cha Uanahabari katika Shule ya Upili ya St...

Kipa Kasper Schmeichel ajiunga na Nice baada ya kuondoka...

T L