Kibarua kigumu mrithi wa Natembeya akianza kazi

Kibarua kigumu mrithi wa Natembeya akianza kazi

Shughuli tele zinamsubiri Mohamed Maalim, mrithi wa aliyekuwa Kamishna Mshirikishi wa eneo kubwa la Rift Valley, George Natembeya anapoanza kazi wiki hii.

Bw Natembeya alijiuzulu Jumatano iliyopita ili kugombea kiti cha ugavana cha Kaunti ya Trans Nzoia kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Bw Maalim alikuwa Kamishna wa Kaunti ya Makueni.Miongoni mwa masuala atakayoangazia akianza majukumu yake kama Kamishna Mshirikishi wa Rift Valley ni kudumisha utulivi wakati wa kampeni za uchaguzi katika kaunti 14 za eneo hilo.

Kupandishwa cheo kwake kumepokelewa kwa hisia mseto na viongozi, wakazi na watalaamu wa masuala ya usalama.Kulingana na Bw Jesse Karanja, mkazi wa Nakuru, Bw Maalim atalazimika kuwa kama Bw Natembeya.

“Eneo hili ni kubwa kutoka Turkana hadi Kajiado na kamishna mshirikishi mpya ni lazima awe tayari kukabiliana na changamoto nyingi za usalama eneo hili. Juu ya yote, atalazimika kuongoza makamishna wote wa kaunti 14 kudumisha ushirikiano,” akasema.

  • Tags

You can share this post!

Treni ya mizigo hadi Uganda kuanza Machi

Namna ya kuondoa harufu mbaya kwenye viatu

T L