Kibarua kizimbani kwa kuteka nyara msichana na kumpapasa matiti

Kibarua kizimbani kwa kuteka nyara msichana na kumpapasa matiti

Na RICHARD MUNGUTI

KIBARUA mwenye umri wa miaka 27 alishtakiwa Jumatano kwa kumteka nyara msichana mwenye umri wa miaka 10.

Boniface Odera Ongwena alikanusha mashtaka mawili mbele ya Hakimu Mkuu Francis Andayi .

Shtaka la kwanza dhidi ya Bw Odera aliyesomewa mashtaka kwa lugha la Dholuo lilisema kati ya Januari 2 na Machi 11, 2018, katika mtaa wa Kasabuni eneo la Ruaraka kaunti ya Nairobi alimteka nyara msichana mwenye umri wa miaka 10.

Shtaka la pili lilisema mshtakiwa alidhulumu kimapenzi mtoto huyo kwa kumpapasa matiti yake.

Mshtakiwa aliomba aachiliwe kwa dhamana.

Hakimu Andayi aliamuru mshtakiwa alipe dhamana ya Sh300,000 pesa tasilimu.

Kesi itasikizwa Aprili 11, 2018.

You can share this post!

Wachuuzi Nairobi waandamana kupinga kuhangaishwa na askari...

EABL yalenga kuunda lita milioni 100 za ‘Keg’...

adminleo