Michezo

Kiboko azima ndoto ya mwanariadha kushiriki mbio za Turkey

October 4th, 2020 1 min read

NA MWANDISHI WETU

Mwanariadha anauguza majeraha mabaya baada ya kuvamiwa na kiboko alipokuwa akifanya mazoezi eneo la Manguo, Nyahururu.

Edwin Mokua wa miaka 28 alikuwa akifanya mazoezi uwanjani karibu na mto Ewaso Nyiro Jumatatu jioni wakati mnyama huyo alimvamia.

Mwanariadha huyo ambaye alikuwa aondoke nchini kueleka Turkey Jumatano aliumizwa mbavu na anapokea matibabu kwenye hospitali ya Nyahururu.

Mokua alikuwa ashiriki kwenye mbio za Marathon Jumapili. Miriam Wangare ambaye alikuwa asafiri naye aliambia Taifa Leo kwamba Mokua alikuwa ashiriki kwenye mbio hizo mara ya kwanza.

Mokua ambaye aliokolewa na wanariadha wenzake Dennis Kipkoskei alisema kwamba alikuwa mita kadhaa mbele yake alipokabiliwa na viboko waliokuwa malishoni.

“Nilipita karibu na Wanyama hao lakini nilipoangalia nyuma sikumuona Mokua,” alisema Kipkoskei.

Alieleza: “Nilimuona akijaribu kujikwamua kutoka kwa kiboko mmoja. Niliwashtua viboko wengine kabla ya kumuokoa kutokana na kibko aliyekuwa amemkabili”.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA