Kibwana, spika kupokea maoni kuhusu BBI

Kibwana, spika kupokea maoni kuhusu BBI

Na PIUS MAUNDU

GAVANA wa Makueni, Prof Kivutha Kibwana na Spika wa Bunge la kaunti hiyo, Douglas Mbilu wamepanga hafla mbili tofauti za kupokea maoni ya raia kuhusu mswada wa marekebisho ya Katiba, 2020 (BBI).

Kwenye matangazo mawili tofauti magazetini, Bunge la Kaunti na Afisi ya Gavana zilitoa wito kwa umma kuwasilisha maoni yao kuhusu mswada huo nyakati tofauti.

Pia, Katibu wa kaunti Benjamin Mutie alitangaza Ijumaa kuwa kutakuwa na misururu ya mikutano Jumatano na Jumanne kote katika jimbo hilo kushirikisha umma kwenye mswada huo.

Bunge la kaunti nalo limebuni kamati ya madiwani 11 ambao watachambua mswada huo huku wengi wao wakifurahia tangazo la Rais Uhuru Kenyatta ya kufuta mikopo ya magari kwao na badala yake kuwapa pesa hizo kama ruzuku.

Kwa mujibu wa Bw Mbilu, wananchi, viongozi na wakuu wa kidini watafaakiana kuhusu mswada huo kabla ya kujadiliwa na kupigiwa kura katika Bunge la Kaunti.

You can share this post!

Jinsi madiwani wanavyotishwa kupitisha BBI

KAMAU: Siasa zina uwezo mkuu wa kuijenga au kuibomoa jamii