Siasa

Kidero amtetea Gachagua, ataka aheshimiwe

May 31st, 2024 1 min read

NA GEORGE ODIWUOR

ALIYEKUWA gavana wa Nairobi, Evans Kidero, amejitokeza kumtetea Naibu Rais Rigathi Gachagua, ambaye amekuwa akipigwa vita na baadhi ya viongozi wa UDA.

Dkt Kidero alisema Naibu Rais anastahili heshima kwa sababu ndiye wa pili anayeshikilia afisi ya juu zaidi nchini.

Naibu Rais amekabiliwa na shinikizo kali katika siku za hivi karibuni huku chama tawala kikikumbwa na misukosuko kisiasa.

Gavana wa Nairobi, Johnson Sakaja ni miongoni mwa waliomkashifu Bw Gachagua huku akimweleza Naibu Rais akome kumpiga vita bosi wake, Rais Wiliam Ruto.