Habari Mseto

Kijana atoweka na mahari ya babake

October 8th, 2020 1 min read

NA STEPHEN ODUOR

Mwanamume wa miaka 74  alipigwa na butwaa Kaunti ya Tana River baada ya mwanawe wa miaka 17 kutoweka na ng’ombe waliokuwa wametayarishwa kulipa mahari ya kuoa mke wa nne.

Mzee Ramadhan Mohammed wa Kijiji cha Titila alisemekana kupigwa na mshang’ao baada ya kugundua mwanawe alikuwa ametoweka na mahari.

Mwanamke anayetarajiwa kuolewa ni msichana wa miaka 17. Jamaa zake waliozungumza na Taifa Leo walisema kwamba  kijana alikuwa amepinga wazo la baba yake kuoa mke wa nne.

Mdogo wa kijana huyo alisema wawili hao walikuwa na mzozo kuhusiana na sherehe ilipangwa kufanyika hivi leo  huku dunguye akisema kwamba babayake alikuwa na ubinafsi.

“Dunguyabgu amekuwa akiwasilisha msichana ambaye angependa kuoa mbele ya babayangu lakini babayangu anakataa ni kama kuna wale wanawake anataka sisi tuoe,amekuwa akikataa changuo letu,” alisema kijana huyo.

Alisema kwamba dungu yake alikuwa ameonya baba yake kwamba hangeruhusu harusi hiyo iendelee.

“Hatukuwa na usiku mtulivu Jumapili baada ya baba yangu na dungu yangu kukabiliana, ikafikia mahali baba yangu akamkana kuwa mwanawe,” alisema nduguye.

Kijana huyo wa miaka 17nalisemekana kutoweka kutoka nyumbani Jumanne baada ya kupeleka mbuzi wake malishoni lakini hakurudi nazo.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA