Habari Mseto

Kijana auawa na umeme Nyahururu

November 9th, 2020 1 min read

NA STEVE NJUGUNA NA FAUSTINE NGILA

Kijana wa miaka 16 aliuawa na umeme Jumanne Nyahururu,  walisema maafisa wa usalama.

Kamanda wa polisi wa Geoffrey Mayek alisema kwamba kijana huyo aliyetambulika kama Sammy Kuria aliripotiwa kuwa alikuwa naaunganisha umeme kutoka nyumbani kwao hadi kwa mtambo wa maji Kijiji cha Warero Jumanne jioni wakati ajali hiyo ilitokea.

“Jamaa wake alipata kijana huyo akiwa amelala kando ya mtambo huo na akaripoti kisa hicho kwa polisi,” alisema Bw Mayek.

Polisi walisema kwamba uchunguzi unaendelea ili kubaini kilichosababisha kifo cha kijana huyo.

“Polisi pamoja na maafisa wa Kenya power walitembelea eneo hilo na uchunguzi  unaendelea kubaini  kilichosababisah kifo hicho,”alisema mkuu huyo wa polisi.

Wakazi waliomba waripoti matatizo yeyote ya umeme eneo hilo na kuhepukana na mwuganisho usio ahali wa umeme ili kuhepukana na matukio kama hayo.

Mwili wa kijana huyo ulipelekwa kwenye chumba cha maiti cha Sipili.