Kimataifa

Kijana huyu wa miaka 17 ananikolesha mahaba chumbani, asema ajuza wa miaka 74

January 15th, 2019 2 min read

MASHIRIKA Na PETER MBURU

TENNESSEE, AMERIKA

AJUZA wa miaka 74 ambaye alifunga ndoa na tineja amesifu ndoa yao kuwa iliyo na mapenzi ya hali ya juu, baada ya miaka mitatu tangu wafunge pingu za maisha.

Bi Almeda Errell alifunga ndoa na Bw Garry Hardwick alipokuwa na miaka 17, japo sasa ana miaka 21 na wakawa mume na mke mnamo 2016.

Hiyo ilikuwa baada ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa wiki mbili tu, wakati Garry alimwomba waoane.

Wawili hao walikutana katika hafla ya mazishi ya mwanawe Almeda.

Wawili hao sasa wamesifiana vikubwa baada ya muda huo kwa pamoja, wakieleza mapenzi wanayoonyeshana kuwa “Zaidi ya ndoto.”

Mwanamke huyo haswa amekuwa akisifu ushupavu wa kitandani wa mumewe, ambaye anamzidi kwa miaka 53, akisema unamkumbusha siku za ujanani.

“Kila wakati tunasifiana na kubusu,” Almeda akasema kupitia video katika mtandao wa YouTube.

“Tunafurahia uhusiano wetu, tumepatana tunaopendana na hatuwezi kutaka kupoteza hizi hisia,” akasema.

Wawili hao wanasema kuwa huwa wanaonyeshana mapenzi kwa kwenda kutazama filamu pamoja ama kupelekana chakula mahotelini.

Almeda alisifu ndoa yake ya sasa kuwa kinyume nay a awali ambapo “hakukuwa na mapenzi ya kutosha ama kubusu na kupigana pambaja.”

Hata hiovyo, Garry ni mchanga kuliko mmoja wa wajukuu wa mke wake huyo. Nyanya huyo alisema alivutiwa na “tabasamu la kupendeza” la mvulana mchanga hivyo hadi akampenda.

Lakini hali ya Garry kuwapenda wanawake wazee inasemekana kuwa tabia yake, kwani anaripotiwa kuanza tabia hiyo alipokuwa na miaka minane, wakati alimpenda mwalimu wake.

Mbeleni alikuwa na uhusiano na mwanamke wa miaka 77 lakini uhusiano huo ukawa na matatizo kwani walikuwa wakikosana mara kwa mara.

Mwanamke huyo anasema kuwa walipotaka kuanza mapenzi alimwambia “nina miaka 71. Si mimi ni mzee sana kwako?” lakini Garry kwa ustadi wa mahaba akamshika mkono na kumjibu “umri na tarakimu tu.”

Wiki chache baadaye walioana, japo baadhi ya watu wa familia walipinga. Garry amekuwa akijitetea vikali kuwa ndoa yao imejengwa kwa msingi wa mapenzi ila si pesa kama wengine wanavyodai.

“Inanikasirisha sana kuwa watu wanapenda kupitisha uamuzi kwa namna hiyo,” akasema.