Makala

KIKOLEZO: Mapinduzi tata ya 'serikali'

November 8th, 2019 3 min read

Na THOMAS MATIKO

SIJUI ufahamu wako wa soka upoje na ikiwa wewe ni mfuatiliaji mzuri wa kandanda ya Ulaya basi utakuwa unawafahamu mastraika wawili; raia wa Argentina Maxi Lopez na Mauro Icardi.

Wawili hawa miaka kadhaa imepita walikuwa ni washikaji wa damu damu.

Mambo mengi walifanya pamoja ikiwemo kula ujana. Urafiki wao ulijengeka kipindi Lopez akiwa yupo kwenye ndoa na mkewe wa zamani Wada Nara aliyezaa naye watoto watatu.

Walifunga ndoa 2008 lakini ikaja kuvunjika 2013 baada ya Lopez kugundua kuwa mshikaji wake Icardi alikuwa akimkaza mkewe kimya kimya.

Hapo akaamua kuachana naye Wada na kumjengea chuki Icardi. Mara tu alipoachana naye Icardi akambeba mzima na mpaka sasa ni mke wake.

Haya pia yanatokea kwenye ulimwengu wa Showbizz. Na yamepelekea mastaa kibao kujengeana chuki. Hawa ni baadhi yao tu.

Miaka mitano iliyopita Dimpoz na Diamond walikuwa marafiki wa damu damu. Walikuwa hawaachani. Ndicho kipindi Victoria Kimani alifanikiwa kuwashirikisha kwenye kolabo yake ‘Prokoto’.

Kipindi hiki Diamond na Wema walikuwa kwenye uhusiano japo wa kutemana wakirudiana.

Ghafla Wema alianza kuonekana kuwa karibu na Ommy na hata wakawa wanaposti za kichokozi sana. Kukazuka tetesi kwamba wawili hao ni kama vile walikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Ndiyo mara ya mwisho Ommy aliwahi kuonekana akiwa karibu na Diamond. Japo hawajawahi kuelezea chanzo cha ugomvi wao mpaka leo, ni bayana kuwa mlahaka wao mzuri ulivunjika huku Wema akitajwa kuwa chanzo. Toka hapo Ommy akawa ‘Team Kiba‘.

ANGELINA JOLIE, Vs BILLY THORTON Na LAURA DERN

Angelina ambaye kwa sasa katengana na aliyekuwa mumewe mwigizaji staa Brad Pitt, aliwahi kunukuliwa akisema kuwa hakuna mwanamume anayeweza kumbabaisha.

Pengine ndio sababu kashindwa na maisha ya ndoa huku ndoa yake kwa Pitt ikiwa ni ya tatu kuvunjika. Isitoshe Jolie kathibitisha kuwa akimtaka mwanamume yeyote hata awe mume wa mtu, atampata na ndivyo alivyoishia kusambaratisha uhusiano wa waigizaji mwenzake Dern na Billy.

Billy na Dern walikuwa wamedumu kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa miaka mitatu na hata walikuwa kwenye mchakato wa kufunga ndoa wakiwa tayari wamenunua mjengo pamoja ambao wangeishi baada ya harusi ili kuanzisha familia. Huku wakiendelea na michakato yao, akatokea Jolie na kumchanganya Billy ambaye aliishia kumtema Dern na kufunga ndoa naye 2000. Ndoa hiyo ya ‘wizi’ ilidumu kwa miaka mitatu na kuvunjika.

ANGELINA JOLIE, Vs BRAD PITT na JENNIFER ANISTON

Unaambiwa tabia ni ngozi, baada ya kumtenda Dern, Jolie hakuchoka na tabia zake za michepuko. Miaka miwili tu baada ya kutemana na Billy, Jolie aliibukia penzi moto lililokuwa likitokota kati ya mwigizai mcheshi Jennifer Aniston na Pitt, na kuivuruga vile vile. Aniston na Pitt walikuwa wamedumu kwenye ndoa tangu 2000 hadi 2005 alipotokea Jolie na kuwavunjia nyumba. Ilianza kama utani pale Pitt na Jolie walipochaguliwa kushuti filamu ya Mr & Mrs Smith kipindi Pitt akiwa na mahusiano na Aniston. Kwa mujibu wa mwandishi maarufu wa wasifu wa watu maarufu Andrew Morton, ulikuwa ni mpango wa Jolie kumpokonya Aniston Pitt. Pitt na Jolie walioana 2014 baada ya kutangaza uhusiano wao wakiwa likizoni hapa nchini Kenya, na ndoa hiyo ikadumu kwa miaka miwili hadi ilipovunjika mwaka jana 2016.

JULIA ROBERTS, VS DANNY MODER na VERA STEINBERG

Julia alikutana na mume wake wa sasa Moder mpiga picha 2002 wakati wa kushuti filamu ya The Mexican. Kipindi hicho Moder alikuwa kwenye ndoa na mke wake wa kwanza Vera waliyeoana 1997. Julia alivutiwa na utanashati wa Moder na licha ya kufahamu kuwa jamaa ana mke, alianza kumzengua kwa kumtia kwenye mitego ya vishawishi hadi akampata. Moder alimtema Vera 2002 na mwaka uo huo akamwoa na mpaka leo yupo katika ndoa naye. Kabla ya kumwoa Julia, mke wa zamani wake Moder hakuwa tayari kutia sahihi nyaraka za talaka hivyo kumlazimu Julia kumhonga kwa dola 150,00 (Sh15 milioni) ndiposa akaumwagia wino na kuachana mazima akubali kutia saini barua za talaka hiyo. Na hilo lilipotimizwa, Julia na Moder wakaoana mara moja 2002.

ROBERT PATTINSON, Vs KRISTEN STEWART na RUPERT SANDERS

Pattinson na Stewart staa masteringi wa msururu wa filamu maarufu za ‘Twilight’. Walikuwa wapenzi kwa kipindi cha miaka mitano. Lakini uhusiano huo ulivunjika pale Stewart aliposhindwa kuwa mwaminifu na kuanza kuchepuka na mume wa mtu, mwelekezi wa filamu ya ‘Snow White And The Huntsman’ Rupert, ambayo mrembo huyo alikuwa akiigiza. Sken

Mwigizaji mkongwe Elizabeth aliyeolewa mara nane katika maisha yake, alikuwa na uhusiano na mwigizaj mwenza, Fisher. Fisher alikuwa mume wake wa nne.

Kipindi cha ujana wao wakiwa waigizaji walioaminiwa sana kule Hollywood, Fisher na Debbie walikuwa katika ndoa huku Elizabeth pamoja na mume wake wa wakati huo Mike Todd walikuwa ni marafiki wao wakubwa wa familia hiyo. Kwa bahati mbaya baadaye, Todd alifariki dunia kutokana na ajali ya ndege, na kumwacha Elizabeth mpweke. Hapo Fisher na Debbie wakawa na ukaribu sana na Elizabeth ili kumfariji. Hiki ndicho kipindi Fisher alianza kuchepuka na Elizabeth kuishia kumwacha mke wake Debbie na kumwoa Elizabeth.

Cha kushanganza ni kuwa Debbie aliwasamehe na hata kurejesha urafiki wao uliofikia hatua ya wao kutayarisha filamu ya pamoja These Old Broads 2001. Wote hawa kwa sasa ni marehemu.