Makala

KIKOLEZO: Ngoma ikirindima sana

October 25th, 2019 1 min read

Na THOMAS MATIKO

HERI imkute yeye ila sio mimi, atakwambia mwanamuziki yeyote pale amwonapo mwenzake akitatizika na sauti yake.

Mnamo Septemba 1997 mwanamuziki mkongwe Julie Andrews, mtunzi wa ‘hit’ Do-re-mi alifanyiwa upasuaji wa kooni na madaktari wawili katika hospitali ya Mount Sinai, mjini New York kuondoa uvimbe fulani uliosababishwa na yeye kuimba sana.

Matokeo yake ikawa ni kuharibika kabisa kwa sauti yake asiweze kuimba tena.

Ilimlazimu lejendari huyo mwenye umri wa miaka 84 kwa sasa kusaka njia mbadala ya kujipatia riziki baada ya kupoteza sauti iliyokuwa ikimpa mtaji.

Hivyo ndivyo alivyoishia kuwa mwandishi wa vitabu.

Aliwashtaki madaktari wale lakini tayari madhara yalikuwa yamesababishwa.

Julie ni mmoja kati ya wanamuziki kibao ambao hawakubahatika kutoka salama kutokana na upasuaji wa aina hii.

Wapo wengine kama wafuatao ambao waliponea kwa tundu la sindano na leo wanaishi kwa kumshukuru Mungu.