Michezo

Kikosi cha Gor kitakacholimana na Lobi Stars ya Nigeria 

December 19th, 2018 1 min read

Na CECIL ODONGO

MABINGWA mara 17 wa KPL nchini Gor Mahia Jumatano Disemba 19 walitoa orodha kamili ya wanasoka mahiri watakaotandaza gozi dhidi ya Lobi Stars ya Nigeria kwenye mechi ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Barani Afrika Jumamosi 22 Disemba 2018 uwanja wa Enugu, Nigeria.

K’Ogalo wapo kifua mbele baada ya kuwadhalilisha Lobi Stars mabao 3-1 na wanahitaji sare, ushindi au wapoteze tu kwa mwanya wa bao moja ili kufuzu hatua ya makundi kwa mara ya kwanza katika historia yao.

Hata hivyo iwapo bahati mbaya itawangukia K’Ogalo na wabanduliwe nje ya mchuano huo, bado watakuwa na nafasi nyingine kujiinua katika soka ya kimataifa kwa kuwa watashushwa hadi mechi za kuwania ubingwa wa Kombe la Mashirikisho Barani Afrika. Kariobangi Sharks ndiyo washiriki wa Kenya kwenye michuano ya kipute hicho.

Hiki hapa kikosi kamili:

Walinda lango:  Boniface Oluoch, Fredrick Odhiambo

Madifenda: Wellington Ochieng, Pascal Ogweno, Philemon Otieno, Haron Shakava, Joash Onyango na Shafik Batambuze

Viungo: Boniface Omondi, Francis Kahata, Kenneth Muguna, Erisa Ssekisambu, George Odhiambo, Cercidy Okeyo na Humphrey Mieno. 

Washambulizi: Francis Mustafa, Samuel Onyango na Jacques Tuyisenge,.

Benchi la Kiufundi: Hassan Oktay – Kocha, Zedekiah Otieno – Naibu kocha, Willis Ochieng – Kocha wa makipa, Jolawi Obondo – Meneja wa timu na Frederick Otieno – Daktari wa timu

Maafisa wa klabu: Gerphas Okuku – afisa wa timu, Lordvick Aduda –Afisa Mkuu Mtendaji na Kelvin Elegwa – Mwakilishi wa Shirikisho la soka nchini FKF