• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 8:55 PM
Makwapa yangu yamekuwa meusi

Makwapa yangu yamekuwa meusi

Mpendwa Daktari,

Makwapa yangu yamebadili rangi na kuwa meusi, jambo linalonisababishia aibu. Nimetumia ndimu, chachu na hata dawa ya kusugua meno ili kujaribu kurejesha rangi halisi ya ngozi ya sehemu hii bila mafanikio. Nifanyeje? Tafadhali naomba usaidizi.

Emily, Nairobi

Mpendwa Emily,

Hali hii inafahamika kama acanthosis nigricans, ambapo seli za pigmenti ya ngozi zinajizidisha kupindukia na hivyo kusababisha sehemu iliyoathirika kubadili rangi na kuwa zito. Hii yaweza kutokea kwa makwapa, shingo, kinena na kiwiko, miongoni mwa sehemu nyingine.

Hasa tatizo hili huhusishwa na uzani mzito kupindukia, maradhi ya kisukari, matatizo ya tezi, aina fulani ya kansa, matatizo ya polycystic ovaries na matatizo mengine ya kihomoni.

Unaweza mtembelea mtaalam wa ngozi ili upate dawa zitakazokusaidia kurejesha rangi halisi ya sehemu hii, na hata ikiwezekana upokee matibabu maalum ya laser. Ikiwa kuna kiini kingine kinachosababisha hali hii, basi utatibiwa.

You can share this post!

Faida za matunda aina ya pepino melon

SHINA LA UHAI: Changamoto katika afya ya akili zabainika...

T L