Kilimo bila kemikali kinalipa, Sylvia asimulia

Kilimo bila kemikali kinalipa, Sylvia asimulia

Na MAGDALENE WANJA

Baada ya Bi Sylvia Miloyo kukamilisha masomo yake na kupata shahada katika ujuzi wa Community Developnment na Saikolojia, aliamua aliamua kuafanya ukulima.

Hii ndio ilikuwa ndoto yake tangu zamani. Mnamo mwaka 2009, alianza ukulima kama njia ya kumpa pato lake la kila siku.

Kama wakulima wine, alitumia kemikali mbali alizopata katika maduka ya ukulima ili kuangamiza wadudud shambani.

Baada ya kufanya aina hii ya ukulima kwa muda wa miaka minne, alikuwa tayari amepokea mafunzo na kusoma kwenye mitandao na vitabu, kuhusu madhara ya matumizi ya baadhi ya kemikali.

“Nilianza kuhisi kwamba sikuwa nina ridhika na aina hii ya ukulima japokuwa ilikuwa ikinipa mapato mazuri,” alisema Bi Miloyo.

Hivyo basi, Bi Miloyo aliamua kujihusisha na aina ya ukulima ya kiliko bila kemikali, ambayo hatatumia aina yoyote ya kemikali.

“Niligundua kwamba matumizi ya kemikali yalikuwa chanzo kikuu cha baadhi ya saratani ambazo zinawaathiri watu sio nchini Kenya pekaa bali ata katika mataifa mengine,” aliongeza Bi Miloyo.

Hata hivyo, haikuwa rahisi kubadilisha kutoka kwa aina hio ya kilimo hadi ile isiyotumia kemikali katika mashamba yake mawili yenye ukubwa wa ekari kumi na tano, Limuru (5) na Mai Mahiu (10).

“Kwa kutumia mapato niliyokuwa nayo, nilianza kuwekeza katika kubadilisha shamba langu na kuhudhuria mafunzo mbalimbali kuhusu aina hii ya ukulima,” alisema.

Baadhi ya mimea ambayo anakuza katika shamba lake ni pamoja na mboga za kiasili kama vile Managu , terere ,tsaga, kunde, mito,mrenda, vitunguu, kabichi, mahindi, maharagwe, pilipili, nyanya, karoti na zinginezo.

Aina hizi mbalimbali za mimiea huzikuza bila matumizi ya kemikali zozote.

“Wadudu ambao husaidia katika kuzalisha maua kama vile nyuki hufa wakati mkulima anatumia kemikali kunyunizia mimea,” aliongeza Bi Miloyo.

Bi Miloyo sasa ana maduka katika sehemu mbalimbali ambapo huwauzia wateja wake mapato hayo. Kampeni yake ya ukulima usiotumia kemikali umezaa matunda kwani wakulima wengine sasa atayari wameukubali.

You can share this post!

Amejipata tajiri kwa kuwashonea wateja nguo kwa ustadi mkuu

UEFA Robo Fainali: Bayern vs PSG, Real Madrid vs Liverpool