Kilimo chatengewa Sh60b

Kilimo chatengewa Sh60b

Na MARY WANGARI

SERIKALI imetengea sekta ya kilimo Sh60 bilioni katika bajeti iliyotangazwa jana na Waziri wa Fedha, Ukur Yatani.

Kiasi cha pesa zilizotengewa sekta ya kilimo katika bajeti ya mwaka huu ni Sh7.2 bilioni zaidi zikilinganishwa na Sh52.8 bilioni zilizotengewa sekta hiyo katika bajeti ya mwaka jana.

Akizungumza jana katika Bunge la Kitaifa alipokuwa akisoma bajeti ya 2021/2022, Waziri Yatani alisema fedha hizo zinazodhamiriwa kuimarisha sekta za kilimo, ufugaji na uvuvi zinatazamiwa kufanikisha kwa asilimia 100 chakula cha kutosha na lishe bora nchini.

Katika fedha hizo zilizotengewa sekta ya kilimo, mradi wa kuongeza uzalishaji wa kilimo na kuboresha mikakati ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya anga miongoni mwa wakulima wa mashamba madogo madogo na jamii za wafugaji, ulitengewa kiasi kikubwa zaidi cha pesa cha Sh10.7.

Mradi wa Kitaifa kuhusu Kilimo Mashinani ulifuatia kwa Sh7 bilioni nao wa Kuendeleza Uvuvi na Maendeleo Kijamii ukatengewa Sh3.4 bilioni., Sh3.2 bilioni na Sh2.1 bilioni mtawalia.Sh2.7bilioni zilitengewa Mradi wa Kuimarisha Nafaka Nchini, Sh2.1 bilioni zikatengewa ujenzi wa Kituo cha Uvuvi cha Liwatoni, Sh 1.8 bilioni Mikakati ya Dharura ya Kukabiliana na Nzige nazo Sh1.5 bilioni zikitengewa Mradi wa Unyunyiziaji na Kuongeza Thamani.

Ujenzi wa Kiwanda cha Samaki cha Lamu ulitengewa Sh1.0 bilioni, Mradi wa Chakula na Ukuzaji Mimea Mbalimbali utatumia Sh620 milioni huku Hazina ya Bima kuhusu Mifugo na Mimea ikitengewa Sh529.5milioni.

Waziri Yatani alifafanua kwamba mikakati ya serikali ya kuwapa wakulima vifaa kwa bei ya chini imechangia pakubwa kupunguza gharama ya uzalishaji, na kuwaongezea mapato.“Wakulima wengi zaidi sasa wanapata vifaa vya kilimo kwa bei ya chini ili kuwapunguzia bei ya uzalishaji na kuimarisha mapato yao,’ akaeleza.

  • Tags

You can share this post!

Bajeti kuipiga jeki miradi yote mikuu ya Pwani

Kilimo chatengewa Sh60b