Kilio cha wakazi wa Kariminu vyanzo vya maji safi vikichafuliwa

Kilio cha wakazi wa Kariminu vyanzo vya maji safi vikichafuliwa

NA LAWRENCE ONGARO

WAKAZI wa Kariminu katika eneobunge la Gatundu Kaskazini waliandamana Ijumaa kulalamikia kuchafuliwa kwa mazingira na kampuni moja.

Walitaja kampuni moja ambayo inajenga bwawa kubwa la maji ili kusambaza katika sehemu tofauti.

Wakazi hao walisema licha ya mradi huo kuendelea mahali hapo lakini kampuni hiyo inaendelea kuchafua mto Kangunu ambao unawafaa kwa maji safi.

Baadhi ya wakazi wa Kariminu wamelalamika kwamba vyanzo vya maji safi vimechafuliwa. PICHA | LAWRENCE ONGARO

Wakazi hao wakiongozwa na Francis Muturi walisema licha ya kutoa malalamiko yao kwa kampuni hiyo pamoja na ile ya Athi River Water Development Authority, bado matakwa yao hayajatatuliwa ipasavyo.

“Uchafuzi wa mto wetu wa Kangunu umetuacha katika hali ngumu kwani tunahofia kuambukizwa maradhi ya tumbo. Tungetaka serikali kuingilia kati ili itusaidie kupata maji safi,” alijitetea Muturi ambaye ni mkazi wa kijiji cha Kariminu.

Bi Maria Njoroge ambaye pia ni mkazi wa kijiji hicho alisema iwapo hatua ya haraka haitachukuliwa bila shaka wakazi wengi watapata maambukizi ya tumbo.

Naibu kamishna wa Gatundu Kaskazini,  Julius Kavita,  ambaye alihutubia wakazi hao wenye hasira, alisema atashauriana na kampuni iliyotajwa, tena haraka iwezekanavyo ili wafanikishe ahadi yao ya kuweka mazingira safi ili majitaka yasichafue mto Kangunu.

Alisema atawasiliana na Mamlaka ya Kuhifadhi Mazingira (NEMA) pamoja na kampuni hiyo ili wapate suluhisho kamili na kusaidia wakazi hao.
  • Tags

You can share this post!

Erling Haaland aongoza Man-City kupepeta Man-United 6-3...

Uhispania yatema idadi kubwa ya wanasoka wazoefu kikosini

T L