KIMANI NJUGUNA: Wakenya wajifunze na kuchagua viongozi wanaofaa mwaka huu

KIMANI NJUGUNA: Wakenya wajifunze na kuchagua viongozi wanaofaa mwaka huu

Na KIMANI NJUGUNA

HATA ikiwa Wakenya wanapenda siasa na kuwachagua viongozi katika nchi nzima, inaonekana baadhi yetu tunawachagua wale ambao kazi yao ni kujitajirisha badala ya kufikiria maendeleo ya maeneo yao.

Ni kwa sababu ikiwa Wakenya wanatarajia maendeleo kutoka kwa serikali za kaunti mwaka huu wa mwisho kabla ya uchaguzi, wataambulia patupu.

Kaunti zote zilitumia karibu kila senti kujilipa mishahara badala ya miradi ya maendeleo.

Kulingana na ripoti ya punde ya Makaguzi wa Bajeti, jumla ya kaunti 22 hakuzitumia hata shilingi moja kufadhili maendeleo, licha ya kutia mifukoni mabilioni ambayo zilipokea na hata kushindwa kuokota ushuru kwa viwango vinavyofaa.

Ripoti hiyo iliyodadisi jinsi kaunti zilitumia pesa za bajeti miezi mitatu ya kwanza mwaka 2021/22, inaonyesha kuwa kwa jumla kaunti zilitumia asilimia 93 ya pesa kwa mishahara na marupurupu, huku mirandi ya maendeleo ikitengwa chini asilimia sita pekee.

Utumizi wa pesa unaonyesha kuwa asilimia 93.3 ya matumizi yote yalienda kwa mishahara na marupurupu.

Pesa hizo ni ongezeko la sh14 bilioni ikilinganishwa na sh35.8 bilioni ambazo kaunti zilitumia kwa mishahara na marupurupu kipindi sawa na hicho mwaka 2020/21.

La kushangaza ni kuwa ni kaunti tatu pekee, Kitui, Kakamega na Kisii ambazo zinaripotiwa kuwa zilitengea miradi ya maendeleo kiwango cha pesa cha kuridhisha kwa kati ya asilimia 8 na 12 ya bajeti zao.

Kwa upande wao kaunti za Mandera, Siaya na Narok aidha zilitumia kati ya asilimia 20 na 28 ya matumizi yote kipindi hicho kufadhili maendeleo.

Ripoti hiyo inatuonyesha kuwa uongozi wa kaunti ni duni kwa vile kinyume na sheria kuhusu usimamizi wa pesa za umma, kaunti zilishindwa kukusanya ushuru kwa kiwango kinachofaa ili kuendesha majukumu yao.

Ni vibaya kuona ripoti hiyo ikifichua kuwa wawakilishi wadi (MCAs) kati ya Julai na Septemba walijilipa Sh57 milioni kwa marupurupu ya kushiriki vikao.

Pesa hizo ni zaidi ya kiwango walichopokea katika kipindi sawa mwaka 2020/21.

  • Tags

You can share this post!

Masomo yatatizika Lamu shule zikiwahifadhi waliokwepa...

Wahalifu wavuruga shughuli za kupata riziki vijijini Lamu

T L