Afya na Jamii

Kinachosababisha uvimbe kwenye sehemu za siri za akina dada

February 26th, 2024 1 min read

NA PAULINE ONGAJI

Kama mwanamke, kuna uwezekano wa wakati mmoja kukumbwa na uvimbe unaojitokeza kila mara kwenye sehemu za siri.

Ni jambo ambalo huwapa wengi wasiwasi. Kuna mambo kadha wa kadha ambayo yaweza sababisha hali hii. Kwa mfano, majipu haya yaweza tokana na maambukizi kwenye vinyweleo.

Maambukizi haya huenda yakatokea wakati wa kunyoa nywele za sehemu nyeti.

Pia, kuna baadhi ya akina dada wanaokumbwa na shida hii pengine kutokana na kinga mwili dhaifu au kwa sababu ya mabadiliko ya kihomoni kama vile mambo yanavyoshuhudiwa wakati wa hedhi.

Tatizo hili pia huwakumba watu wenye uzani mzito.

Wakati mwingine uvimbe huu hukoma bila tiba yoyote na kuacha makovu.

Kumbuka kwamba hali hii haiambukizani na haisababishwi na viwango duni vya uchafu, kumaanisha kwamba haipaswi kukuingiza kiwewe.

Hata hivyo, ikiwa hali hii itaendelea kwa wiki kadhaa utahitaji kumwona daktari au mtaalamu wa ngozi ili upewe viua vijasumu na dawa za maumivu.

Mtaalam huyu atakuelekeza iwapo unahitaji matibabu zaidi.