Kinara wa Arsenal atetea matumizi ya fedha ya kikosi hicho katika soko la uhamisho muhula huu

Kinara wa Arsenal atetea matumizi ya fedha ya kikosi hicho katika soko la uhamisho muhula huu

Na MASHIRIKA

MKURUGENZI wa kiufundi kambini mwa Arsenal, Edu Gaspar, ametetea sera za usajili wa kikosi hicho ambacho kwa sasa kinavuta mkia wa EPL baada ya kupoteza mechi zote tatu za ufunguzi wa msimu huu dhidi ya Brentford, Chelsea na Manchester City.

Chini ya kocha Mikel Arteta, Arsenal walimwaga sokoni zaidi ya Sh24 bilioni na ndicho kikosi kilichotumia fedha nyingi zaidi kuliko washiriki wote wengine wa EPL.

“Tutazame hali hiyo kwa muktadha mpana zaidi kuliko kiasi cha fedha. Tulisajili wanasoka sita walio chini ya umri wa miaka 23. Taratibu zetu ziliongozwa na mpango wa siku za baadaye. Mpango huo umekuwepo kwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita,” akasema.

Beki raia wa Uingereza, Ben White ndiye sajili ghali zaidi wa Arsenal muhula huu baada ya kushawishiwa kuondoka Brighton kwa Sh7.8 bilioni.Arsenal walisajili pia wanasoka Albert Sambi Lokonga, Martin Odegaard, Aaron Ramsdale, Nuno Tavares na Takehiro Tomiyasu.

Kikosi hicho hakishiriki soka ya bara Ulaya muhula huu kwa mara ya kwanza tangu 1995 na mwanzo wao katika EPL muhula huu ndio mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 67.

  • Tags

You can share this post!

Ufaransa yateleza tena huku Uholanzi ikitamba katika mechi...

Ngilu ahimiza Kalonzo amuunge Raila mkono