Kinda wa Gor Mchezaji Bora Oktoba

Kinda wa Gor Mchezaji Bora Oktoba

Na CECIL ODONGO

BEKI wa kati wa Gor Mahia, Frank Odhiambo (pichani) jana alituzwa kama Mchezaji Bora wa Oktoba wa timu hiyo katika hafla ya kipekee iliyoandaliwa ugani Camp Toyoyo, Nairobi.

Kutokana na ufanisi huo, beki huyo mwenye umri miaka 19, alituzwa Sh25,000 kutoka kwa wadhamini wa K’Ogalo, Betsafe.Alikabidhiwa tuzo hiyo na Afisa Mkuu Mtendaji wa Betsafe Vincent Simiyu baada ya mazoezi ugani humo. Kuhusu mechi ya K’Ogalo dhidi ya AS Otoho d’Oyo, Odhiambo alisema licha ya wachezaji wao 16 pekee kwa mechi hiyo, timu hiyo ina uwezo wa kuwapiga wageni wao na kutinga hatua ya makundi ya Caf.

Beki huyo wa kati amekuwa tegemeo kwa Gor katika safu ya ulinzi tangu achezee mara ya kwanza mnamo Mei 2021 dhidi ya Nairobi City Stars katika mechi ya ligi.“Nashukuru familia ya Gor, makocha na wachezaji kwa sababu bila wao, singeweza kushinda tuzo hii.

Pia ningependa kuwashaajisha wadhamini wetu Betsafe waendelee kutoa tuzo hizi kwa sababu zinatupa motisha,” akasema Odhiambo.Simiyu naye alipongeza Gor kwa mwanzo mwema wa msimu wa 2021/22 ambapo bado hawajapoteza mechi yoyote huku wakiwa kileleni mwa jedwali kwa alama 16 baada ya mechi nne.

“Wachezaji wa Gor wamejituma na kupata matokeo mazuri msimu huu. Kama wadhamini wenu tunafurahia sana ufanisi huu na nawarai wachezaji waendee Congo ili wapate matokeo mazuri. Nawatakia mema,” akasema Simiyu

You can share this post!

Simbas wahitimisha ziara na Wahispania

KPA yavizia Equity na kuponyoka na ‘mali’

F M