Kimataifa

King'asti auza ubikira mtandaoni akidai hajapata ‘Mr Right’

September 7th, 2018 1 min read

Na Geoffrey Anene

MWANAMKE mmoja Mjerumani kwa jina Mandy amefanikiwa kunadi ubikira wake kwenye mtandao wa kijamii kwa Sh29,310,411.

Mandy, 36, ambaye ni mhudumu katika ndege, aliomba msaada wa kuuza ubikira wake kutoka kwa shirika la Cinderella Escorts kwenye mitandao baada ya kupata tovuti ya shirika hilo katika gazeti moja, na ubikira wake sasa umenunuliwa na mwanabishara mmoja ambaye hakujitambulisha jijini Munich, gazeti la Daily Mail limeripoti.

Kichuna huyo, ambaye azma yake ni kuwa mwanamuziki, alisema aligundua hawezi kupata mwanamume wa ndoto yake na kuambia gazeti la Daily Mail aliamua kutofanya mapenzi. “Kupata mwanamume anayeafiki ndoto yangu ni sawa na kucheza karata. Nimesubiri miaka mingi.”

Na Mandy, ambaye amesema kwamba atatumia mapato ya mnada huo kuimarisha taaluma yake na kusaidia familia yake, amefichua kwamba ubikira katika umri huo wake ulichangia kitita hicho kikubwa.

“Kila mwanamke anaweza kupoteza bikira mara ya kwanza tu,” alisema Mandy, ambaye atakutana na mnunuzi huyo ili kukamilisha mnada huo mwezi huu wa Septemba.

Bado kipusa huyu hajakataa tamaa kabisa ya kukutana na mwanamume wa ndoto yake.

Wakili na mwanasoka mmoja walishikilia nafasi ya pili na tatu katika mnada huo wa ubikira wa Mandy kwa Sh28,082,979 na Sh23,402,482, mtawalia.