KINYANG’ANYIRO 2022: Kaunti ya Kajiado

KINYANG’ANYIRO 2022: Kaunti ya Kajiado

NA STANLEY NGOTHO

KAJIADO ni kaunti ya nane kwa ukubwa nchini baada ya Turkana, Marsabit, Wajir, Garissa, Tana River, Isiolo na Kitui.

Inapakana na Kaunti ya Narok upande wa Magharibi, Nakuru, Kiambu, Nairobi upande wa Kaskazini, Machakos, Makueni, Taita-Taveta kwa upande wa Mashariki na nchi ya Tanzania kwa upande wa Kusini.

Mpaka mkubwa wa Kenya na Tanzania katika kaunti hii ni Namanga. Pia kuna mpaka wa Loitoktok.

Baadhi ya miji inayopatikana katika kaunti hii ni Ongata Rongai, Kitengela, Ngong, Kajiado, Kiserian, Loitokitok, Namanga, Isinya na Ilbisil.

Baadhi ya watu mashuhuri waliolitoka Kajiado ni waliokuwa mawaziri Stanley Oloitiptip, John Keen, Geofrey Parpai na aliyekuwa makamu wa Rais Profesa George Saitoti.

Kaunti hii ina maeneo kadhaa ya utalii ikijumuisha Mbuga ya Amboseli, Ngong Hills, chemichemi ya Mzima, Ziwa Magadi, Ziwa Natron, eneo la kihistoria la Olorgesailie, mbuga ya Chyulu, Makavazi ya Maasai, Mbuga ya Wanyama ya Tsavo Mashariki na kadhalika.Wakazi wa Kajiado wanategemea ufugaji wa mifugo na kilimo.

CHANGAMOTO: Wakazi wanamtaka kiongozi ambaye atawaunganisha jamii, kuboresha elimu, kuwekeza katika sekta ya maji, miundomsingi na ugawaji sawa wa rasilimali na mazingira mazuri ya kufanya biashara.

KAJIADO: Ni Kaunti nambari 34

UKUBWA: Kilomita 21,292.7 mraba.

IDADI YA WATU: 1,117,840 kulingana na Sensa ya 2019.

WAPIGA KURA: 453,372

MAENEO BUNGE: Kajiado Kusini (wapiga kura 69,298) Kajiado Kati (wapiga kura 63,684), Kajiado Mashariki (wapiga kura 114,177), Kajiado Magharibi (wapiga kura 64, 026) na Kajiado Kaskazini (wapiga kura 142,187).

Gavana wa sasa ni Joseph Jama Ole Lenku ambaye anatetea kiti chake kupitia tikiti ya ODM.

Kajiado ina maeneo kadhaa ya utalii ikijumuisha Mbuga ya Amboseli, Ngong hills, chemichemi ya Mzima, Ziwa Magadi, Ziwa Natron, eneo la kihistoria la Olorgesailie, mbuga ya Chyulu, mbuga ya Maasai, Tsavo Mashariki na kadhalika.

Wakazi wanategemea ufugaji wa mifugo na kilimo. Wakazi wanamtaka kiongozi ambaye atawaunganisha jamii, kuboresha elimu, kuwekeza katika sekta ya maji, miundomsingi na ugawaji sawa wa rasilimali na mazingira mazuri ya kufanya biashara.

UGAVANA

JOSEPH JAMA OLe LENKU

Ana umri wa miaka 52

Anatetea kiti chake kupitia tikiti ya ODM

Ole Lenku ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Nairobi, ambapo alipata Shahada ya Uzamili katika masuala ya Biashara katika usimamizi wa kimkakati na Shahada ya Biashara katika Masoko.

Amefanya kazi kama meneja katika baadhi ya hoteli nchini na Tanzania. Mnamo Mai 23, 2013, Ole Lenku alichaguliwa kuwa Waziri wa Ndani katika serikali ya Rais Uhuru Kenyatta.

Mwaniiaji mwenza wake Martin Moshisho,37. MANIFESTO: Kuimarisha sekta ya afya, elimu, miundomsingi, kilimo, ufugaji na kuwaunganisha wakazi wa Kajiado.

DKT DAVID NKEDIANYE

Ana umri wa miaka 59

Aliyekuwa gavana wa kwanza wa Kaunti ya Kajiado kati ya 2013- 2017 kupitia tikiti ya ODM

Amewahi kuwa mwalimu wa Shule ya Upili

Ana Shahada ya PhD katika Ufugaji, matumizi ya ardhi na uhifadhi kutoka Chuo Kikuu cha Edinburgh.

Dkt Nkedianye pia ana digrii ya Elimu Jamii na maadili kutoka Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afrika Mashariki.

MANIFESTO: Kuimarisha sekta ya elimu, maji, afya, miundomsingi na mazingira.

Mwaniaji mwenza wake ni Joseph Manje,60.

JUDAH KATOO OLE METITO

Ana umri wa miaka 50

Ni mbunge wa Eneobunge la Kajiado Kusini

Atawania kiti hicho kwa tikiti ya UDA

Ana shahada ya B.Sc. katika Teknolojia ya viwanda kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi

Alihudumu kama waziri wa usalama wa ndani kati ya 2012-2013 chini ya utawala wa Rais Kenyatta kufuatia kifo cha Profesa George Saitoti.

Mwaniaji mwenza wake ni Judy Muthoni, 32.

MANIFESTO: Anaahidi kuboresha sekta ya afya, uunganishaji wa maji na kukuza uchumi wa Kajiado.

PETER AMBROSE NG’ANGA KAGO

Ana umri wa miaka 63

Mwaniaji huru

Alikuwa diwani wa wadi wa Kiserian kati ya 2002 -2007.

Ana shahada ya kwanza katika usimamizi wa umma kutoka Chuo Kikuu cha KCA. Pia MA katika ujasiriamali kutoka Chuo Kikuu cha JKUAT.

Mwaniaji mwenza wake ni Robert Njonjo

MANIFESTO: Anaahidi kusuluhisha suala la maji na kuhakikisha kuwa mali ya umma inatumika kwa njia inayofaa.

USENETA

Judith Pareno (ODM)

Wakili

Anahudumu kama seneta maalum

Amewahi kuhudumu kama mbunge wa EALA kati ya 2013-2017.

Aliwahi kuwa mkurugenzi wa uchaguzi wa chama cha ODM.

Moses Sakuda (Jubilee)

Mtaalamu wa maendeleo ya uchumi wa jamii

Ni mbunge wa zamani wa maeneo bunge ya Kajiado Kaskazini na Magharibi.

Aliwahi kuwa makamu mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya Mendeleo ya Ewaso Nyiro Kusini (Esida) kwa miaka mitatu baada ya kupoteza kiti chake mnamo 2017.

Samuel Seki Kanar (UDA)

Aliyekuwa mtumishi wa umma Kaunti ya Kajiado kati ya 2013-2017

Alikuwa waziri wa Kaunti ya Narok.

Gideon Toimasi almaarufu Kagame, 27 (Wiper)

Mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Nairobi, anasomea masuala ya siasa.

Simon Peter Ole Nkeri

Mtaalamu wa masuala ya pesa

Alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya East Africa Portland Cement.

Alikuwa meneja mkuu wa Hazina ya Kitaifa ya Mafao ya Uzeeni (NSSF) Mnamo 2003, kwa muda mfupi alifanya kazi kama Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Soko la Mitaji (CMA).

Pia amefanya kazi katika Benki ya Barclays ambako alikuwa mkuu wa huduma za kibiashara.

UBUNGE

KAJIADO KASKAZINI

1. Onesmus Ngogoyo (UDA)

2. George Yogo (ODM)

3. Francis Parsimei Gitau (Jubilee)

4.Martin Kimemeia (Huru)

6. Paul Kibathi (PPK)

7. Nicholas Teka (Huru)

8.Anita Soina (Green Party)

9.Andrew Nyangwasa (Huru)

KAJIADO MASHARIKI

1. Kakuta Mai Mai (ODM)

2.Marina Kelly (Jubilee)

3.Mary Seneta (UDA)

4.George Kingori (TSP)

5.Samuel Maingi (Saris) (Chama cha Kazi)

6.Douglas Keton (Huru)

KAJIADO KUSINI

1.Parashina Sakimba (ODM)

2. Samuel Kututa (UDA)

3. John Parit (Jubilee)

4.Daniel Nina Livondo (PNU)

5.Elijah Naini (Huru)

KAJIADO MAGHARIBI

  1. Konana (ODM)
  2. Joseph Simel (Jubilee)
  3. George Sunkuiya (UDA)
  4. Jacob Wangai Gitau (PPK)

KAJIADO KATI

1.Elijah Memusi (ODM)

2.Moses Birisha (Wiper)

3 Antony Keroken (Jubilee)

 

WAWANIAJI WA NAFASI YA MBUNGE MWAKILISHI WA KIKE

Jenipher Moinkett Meeli (ODM)

Wakili na mtetezi wa haki za watoto

Anaahidi kuwapa nafasi sawa watu wanaoishi na ulemavu

Leah Sopiato Sankaire (UDA)

Anawania kwa mara ya kwanza

Ana digrii ya usimamizi wa miradi kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.

Anaahidi kukuza maslahi ya wanawake na watoto

Simayiai Rakita (Jubilee)

Mhitimu wa mawasiliano na mfanyabiashara

Aligombea nafasi hiyo mnamo 2017 lakini akashindwa.

Anaahidi kuhakikisha mali ya umma inatumika kwa njia inayofaa.

Wacuka Mathenge (TSP)

Kwa sasa anahudumu kama diwani maalum katika bunge la Kaunti ya Kajiado.

Aligombea kiti hicho 2013 lakini akashindwa.

Alihudumu kwa miaka 13 kama mweka hazina wa muungano wa matatu nchini.

Anaahidi kutetea miradi ya makundi yaliyotengwa katika kaunti.

  • Tags

You can share this post!

CHARLES WASONGA: IEBC ifafanue masuala tata mapema kuhusu...

Mwendeshaji baiskeli Kariuki atawala Migration Gravel Race...

T L