KINYANG’ANYIRO 2022: Kaunti ya Laikipia

KINYANG’ANYIRO 2022: Kaunti ya Laikipia

NA STEVE NJUGUNA

KAUNTI ya Laikipia ni mojawapo ya kaunti 47 nchini Kenya ambayo iko katika eneo la Bonde la Ufa.

Kati ya watu wa kaunti hii 259,440 ni wanaume, 259,102 wakiwa ni wanawake na 18 wakiwa ni watu wa jinsia mchanganyiko yaani huntha (intersex persons).

Gavana wa sasa ni Ndiritu Muriithi ambaye kwenye uchaguzi mkuu wa 2017 alichaguliwa kama mgombea huru na anatafta fursa ya pili Agosti 9 na tiketi ya chama cha Jubilee.

Ina maeneo bunge matatu: Laikipia Magharibi ndilo ndilo eneo ubunge kubwa na lenye wapiga kura wengi zaidi linawakilishwa bungeni na Patrick Kariuki Mariru (Jubilee) lina wadi sita (6); Igwamiti, Ol-Moran, Rumuruti mjini, Githiga, Marmanet and Salama.

Laikipia Mashariki ina wadi tano: Ngobit, Tigithi, Thingithu, Nanyuki and Umande. Mbunge wa sasa ni Amin Deddy Mohammed Ali anayetetea kiti kupitia UDA.

Laikipia Kaskazini ina wadi nne; Sosian, Segera, Mugogodo Magharibi na Mugogodo Mashariki. Mbunge wa sasa ni Sara Paulata Korere anayetetea wadhifa kupitia Jubilee.

Kaunti hii ni nyumbani kwa watu kutoka jamii mbali mbali ina miji miwili mikuu: Mji wa Nanyuki upande wa kusini-mashariki, na Mji wa Nyahururu upande wa kusini-magharibi. Makao makuu ya kaunti yako katika Mji wa Rumuruti.

Kaunti ya Laikipia in mojawapo ya kaunti zinazotajwa kuwa kati ya vivutio vya utalii wa nyika na wanyamapori barani Afrika.

Shughuli za kiuchumi katika kaunti hii zinajumuisha utalii, kilimo, hasa mazao ya nafaka, ufugaji wa mifugo na kilimo cha bustani chafu (greenhouse horticulture).

CHANGAMOTO: Utovu wa usalama unaochangiwa na wezi wa mifugo, kutoka kaunti jirani za Baringo, Samburu na Isiolo. Kuna ukosefu wa maji, migogoro kati ya binadamu na wanyamapori, upatikanaji wa soko za mazao ya shambani na mifugo, upatikanaji wa elimu kwa watoto kutoka katika jamii za wafugaji, ndoa za mapema na Ukeketaji.

UGAVANA

NDIRITU MURIITHI – Jubilee

Ni gavana wa pili aliyeingia 2017.

Alizaliwa Februari 10, 1967, (ana umri wa miaka 55).

Ana shahada ya kwanza ya Uchumi (B.A) kutoka Chuo kikuu cha St Francis Xavier, Canada na shahada ya uzamili katika usimamizi wa miradi na masharika (M.A) kutoka Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Australia, Sydney.

Amedumu siasani kwa miaka 20.

Alichaguliwa mbunge wa Laikipia

Magharibi kupitia chama cha PNU 2008 hadi 2013 aliposhindwa ugavana na mtangulizi wake Joshua Irungu.

Alihudumu kama Naibu waziri wa Viwanda (2008-2013) chini ya serikali ya muungano.

MANIFESTO: Upatikanaji wa maji safi na ya uhakika kwa kila mkaaji, huduma bora za afya na nafuu, kuongeza ajira zaidi kwa vijana, kuboresha barabara na miundo msingi katika vituo vya kibiashara na ulinzi wa maisha na mali.

JOSHUA WAKAHORA IRUNGU – UDA/ Kenya Kwanza

Alizaliwa Januari 1, 1970 (ana umri wa miaka 52).

Ni gavana wa kwanza wa Laikipia kati ya 2013 hadi 2017.

Alijitosa siasani 2013 na kushinda kiti cha ugavana kupitia chama cha TNA.

Ana shahada ya sanaa (B.A) ya Usimamizi wa maliasili na shahada ya Uzamili ya Kilimo na Maendeleo ya Jamii kutoka chuo kikuu cha Egerton.

Kabla ya siasa, aliwahi kuhudumu kama mtumishi wa umma katika Wizara ya Kilimo akisimamia maafisa wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo wilaya ya Laikipia kabla ya kujiuzulu kutoka serikalini na kujiunga na USAID, kama msimamizi wa kikundi cha International Small Group and Tree planting programme (ISGTPP).

Mnamo 2019 aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Udhibiti wa Huduma za Maji (WASREB) ambapo amehudumu kwa kipindi cha miaka mitatu.

MANIFESTO: Afya bora, ajira

kwa vijana, kuboresha kilimo, upatikanaji wa soko kwa mazao na mifugo na kufufua uchumi (The Bottom Up Approach).

JOSPHAT GITONGA KABUGI (NARC-Kenya)

Alizaliwa Novemba 22, 1966, (ana umri wa miaka 56).

Ni mhandisi, Mshauri wa Fedha na Ushuru akiwa amesomea Shahada ya Sayansi katika Uhandisi wa udongo na maji kutoka Chuo Kikuu Cha Windsor, Canada.

Alijiunga na siasa mwaka wa 2013 na kuwa naibu wa gavana wa kwanza wa Laikipia chini ya serikali ya Joshua Irungu.

MANIFESTO: Kukuza utalii, afya bora, kuinua kilimo, kuimarisha miundo misingi, kuinua elimu, kuimarisha usalama, upatikanaji wa maji safi na kupiga jeki biashara na uwekezaji.

RICHARD MBURU KAMAU (Huru )

Alizaliwa 1960, (miaka 62).

Ni mwekezaji katika sekta ya utali na mikahawa akiwa amesomea Shahada ya Biashara katika uhasibu na Uchumi kutoka Chuo Kikuu Cha NAGPUR, India

Pia ni mhasibu wa Umma aliyeidhinishwa katika Chuo Kikuu cha Strathmore.

Alijiunga na siasa mwaka wa 2013 na kupigania ugavana lakini akaibuka wa nne.

Kabla ya kujiunga na siasa aliwahi kuhudumu kama mhasibu mkuu katika shirika la serikali la New- KCC.

MANIFESTO: Kukuza utalii, afya bora, kuinua kilimo, kuimarisha miundo misingi, kuinua elimu, kuimarisha usalama, upatikanaji wa maji safi na kupiga jeki biashara na uwekezaji.

MBUNGE MWAKILISHI WA KIKE

JANE WANGECHI KAGIRI – (UDA)

Ni mjasiliamali na mmiliki wa kampuni Creativedge Solutions inayohusika na ujenzi, suluhu za IT, zabuni za vifaa vya kuandikia miongoni mwa zingine.

Jane Wangechi Kagiri anayewania uwakilishi wa kike wa Laikipia. PICHA | STEVE NJUGUNA

Aliwahikuhudumu kama mshauri wa masuala ya vijana, wanawake na ICT wa Generali Mohamed Badi ambaye ndiye mkurugenzi mkuu wa huduma ya jiji la Nairobi.

VIRGINIA WAMBUI NDERITU – (Jubilee)

Ni mwanaharakati wa jinsia.

Alihudumu kama waziri wa barabara na mashamba katika serikali ya kwanza ya kaunti ya Laikipia.

Hii ndiyo mara yake ya tatu kukipigania kiti hiki.

JANE WANJIRA APOLLOS – (Huru)

Ndiye mbunge mwakilishi wa wanawake wa kaunti ya Laikipia aliyechaguliwa kwenye tiketi ya TNA.

Ana Shahada ya Kwanza ya Sanaa katika Ushauri kutoka chuo cha UGSC, North Carolina.

Alishindwa kwenye uchaguzi wa 2017 alipokipigania kiti hicho kama mgombea huru dhidi ya mbunge wa sasa Catherine Waruguru.

PURITY KENDI GITONGA – (Huru)

Alizaliwa Umande, Laikipia Mashariki.

Ana Shahada ya biashara katika fedha.

Ni mwanaharakati wa jinsia.

Aliibuka wa pili kwenye uchaguzi wa mchujo baada ya kuzoa kura 23,154 dhidi ya Bi Jane Kagiri aliyezoa 28,978.

Hata hivyo, Bi Gitonga ambaye alidai kuwa zoezi hilo lilikumbwa na utovu wa nidhamu alipinga matokeo hayo na kuwasilisha malalamishi kwa Kamati ya Mizozo ya Uchaguzi na Maamuzi.

Hata hivyo malalamishi yake yalitupiliwa mbali.

UBUNGE

LAIKIPIA MAGHARIBI

Stephen Wachira Karani – UDA

Sarolyne Mwendia – Jubilee

Ibrahim Ngugi Kagombe – TSP

John Karanja Waithira –Narc K

Cecilia Wairimu Gichuhi –PNU

John Mathenge- USAWA

Charles Gachema – GCP

David Ndichu Gitau – (Huru)

George KAMAU Kamatu- (Huru)

Wallace Ndiritu Kariuki – (Huru)

Eston Maina – (Huru)

Mathew Mathenge- (Huru)

David Mugo Ndumia – (Huru)

Ben Kang’ara – (Huru)

LAIKIPIA MASHARIKI

Amin Deddy Mohammed Ali (UDA)

Mwangi Kiunjuri – TSP

Anthony Rukwaro – Jubilee

David Njoroge – Huru

Philip Ndegwa – The New Democrat

Simon King’ori – ODM

LAIKIPIA KASKAZINI

Sara Paulata Korere – (Jubilee)

Mathew Lemprukel – (ODM)

Maina Munene – (UDA)

Gabriel Lorere (UPIA)

Timothy Musiany – (Huru)

USENETA

JOHN NDERITU KINYUA (UDA)

Ndiye senata wa sasa wa kaunti ya Laikipia aliyechaguliwa mara mwaka wa 2017 kupitia chama cha Jubilee.

Alizaliwa Julai 16, 1975 (Ana umri wa miaka 47).

Ana Shahada ya Sayansi katika kemia na botania (BSC, CHEMISTRY & BOTANY) kutoka chuo kikuu cha Nairobi.

Alihudumu katika kampuni kadhaa za madawa na maabara hapa nchini kabla ya kujiunga na siasa mwaka wa 2007 alipochaguliwa kama Diwani wa Mutara kaunti ya Laikipia 2007 – 2013.

JOHN MATHENGE MWANIKI (Jubilee)

Ndiye naibu gavana wa sasa.

Ana tajriba ya zaidi ya miaka 20 wa katika nyanja za Habari na Teknolojia (IT) na Fedha akiwa na Shahada ya Biashara na ile ya Uzamili wa usimamizi wa Usimamizi wa biashara (Bachelor of Commerce and Master of Business Administration) kutoka chuo kikuu cha Nairobi.

Pia ana Shahada ya Uzamili ya usimamizi wa Sera za Umma (Master of Public Policy and Management) kutoka Chuo Kikuu cha Strathmore.

Aliwahi kutekeleza kwa ufanisi suluhu za masoko ya fedha katika Benki Kuu ya Kenya, Benki Kuu ya Sudan Kusini, Benki Kuu ya Ushelisheli, Soko la Hisa la Nairobi, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji ya Kenya, Masoko ya Mitaji ya Rwanda na Uunganishaji wa SADC kati ya zingine.

Alihudumu kama katibu wa kaunti na mkuu wa utumishi wa umma katika Kaunti ya Laikipia katika serikali ya kwanza Laikipia kabla ya kuchaguliwa kuwa Naibu Gavana.

Ndiye Mwenyekiti wa Kitaifa wa chama cha Manaibu gavana nchini.

JOHN MAINA NJENGA (KANU)

Alizaliwa Januari 2, 1969 (Ana umri wa miaka 53)

SAM MWANGI THUITA (Narc-K)

Aliwahikuhudumu kama katibu wa kudumu katika wizara ya masuala ya nchi za kigeni chini ya serikali ya marehemu Rais Mwai Kibaki.

Ni wakili aliye na zaidi ya miaka 26 katika utumishi wa umma ambapo alianza kama mwanasheria mchanga.

Alijiunga na siasa mwaka wa 2017 ambapo alikipigania kiti cha cha gavana wa kaunti ya Laikipia laikini akashindwa kwenye uchaguzi wa mchujo wa chama cha Jubilee.

HENRY MBUTHIA KIMANI (Chama Cha Kazi)

Ana shahada ya Uzamili ya usimamiz wa Biashara na Shahada ya Sayansi Katika Uhandisi mitambo.

Alihudumu kama afisa mkuu wa fedha wa serikali ya katika ya kwanza kaunti ya Laikipia.

ROBERT NDUNG’U (ANC)

Ni mtaalam wa masuala ya usalama, Sheria na maendeleo na ana tajriba ya zaidi ya miaka 15 kaika nyanja hizi.

JOHN KIAMA GITHINJI (TSP)

Aliwahi kuhudumu kama Meneja wa Mauzo wa kampuni ya Zenko Kenya Ltd.

Ni mwandani wa karibu wa Kiongozi wa Chama Cha TSP na waziri wa kitambo wa kilimo Mwangi Kiunjuri.

JULIUS MAMAIYO – (ODM)

Anatoka katika jamii la wafugaji zinazoishi katika eneo ubunge la Laikipia Kaskazini

Ndiye mtu wa kwanza kutoka jamii ya wafugaji kukipaginia kiti hiki tangu ujio wa ugatuzi

  • Tags

You can share this post!

Majeshi ya Urusi yateka mji mwingine Ukraine

Muruli aahidi uwazi baada ya kuchaguliwa kuongoza tawi la...

T L