KINYUA BIN KING’ORI: Matamshi ya Ruto kwa hakika yanaweza kumponza Mlimani uchaguzi wa 2022

KINYUA BIN KING’ORI: Matamshi ya Ruto kwa hakika yanaweza kumponza Mlimani uchaguzi wa 2022

Na KINYUA BIN KING’ORI

MBINU mpya ya Naibu Rais, Dkt William Ruto kukabiliana na viongozi wa Mlima Kenya wanaompigia debe kiongozi wa ODM, Raila Odinga anayeaminika kuwa mpinzani wake mkuu katika uchaguzi mkuu ujao, huenda ikamponza kisiasa katika eneo hilo.

Ukweli ni kuwa , Dkt Ruto amevutia hisia za wakaazi wengi katika eneo la Mlima Kenya kiasi cha wengi kujiunga na mrengo wake wa Hustlers Nation, lakini matamshi yake kuwafokea magavana wanaomvumisha Bw Raila huenda yakachochea baadhi ya wafuasi wake kubadilisha msimamo wao na kumnyima kura.

Majuzi akiwa Gatundu Kaskazini, Kaunti ya Kiambu, Dkt Ruto alimfokea vikali Gavana James Nyoro kwa kuunga mkono Bw Raila.Aidha, akiwa Kaunti ya Meru, Novemba 16, 2021, alimshambulia vikali Gavana Kiraitu Murungi akimtaka kukoma kulazimisha jamii ya Ameru kuunga mkono BW Raila maana wananchi ndio watakaoamua kiongozi watakaye awe rais wao.

Je, ikiwa Naibu Rais anajua wananchi ndio watakaoamua mbona basi kuwashambulia kina Kiraitu bure? Japo ni kawaida wanasiasa kutusiana, kupakana tope, kulumbana na kukoseana heshima wakati wa kampeni, Naibu Rais anafaa kukoma kuwaingilia viongozi wengine wasiomuunga mkono katika azma yake ya kuwa wrais.

Kila kiongozi ana jukumu la kuhakikisha jamii yake inaelewa manufaa ya kuunga mkono kiongozi ambaye ataimarisha maendeleo katika eneo lao na nchini akiwa raisHivyo, si kosa la jinai kwa magavana wa Mlima Kenya kuamua wataunga mkono handishake na Raila.

Hivyo, ikiwa katika maoni yao anayestahili kuungwa mkono ni Raila, ni haki yao na inapaswa kuheshimiwaMaoni yao hayafai kuchukuliwa kama msimamo wa jamii.Wala kumfanya Dkt Ruto kuwa mkali na mwenye hasira ya mkizi.

Kwa kuwa Dkt Ruto amevutia umaarufu mashinani,ni jukumu lake kuendelea kudumisha umaarufu huo au akiteleza auporomoshe.kufaulu hilo ni kuwa mpole,mnyenyekevu na kuzidisha kutongoza viongozi wanaompinga si mlimani tu bali kote nchini ili kuwanasa.

Japo Naibu Rais amekuwa akisisitiza amejipanga kushinda Urais mwaka ujao, huenda matamshi yake yakamtia hatarini na kujikuta akichungulia nje ya ikulu 2022.kiburi na majivuno yatamsababishia balaa kisiasa na kufifisha juhudi zake.

Asijione maarufu mlimani kiasi cha kuanza kuwakejeli viongozi wa eneo hilo ambao huenda wakaungana na kutishia umaarufu na kura.Mwaniaji Urais kama Dkt Ruto kutumia muda mwingi kulumbana na kina Murungi ni kujishusha hadhi, washindani wake ni kina Raila odinga, Kalonzo, Musalia mudavadi na wengine.

Kiongozi huyo wa Hustlers Nation anafaa kuachia wafuasi Wake jukumu la kuwakabili viongozi wapinzani wake,ana jeshi la wanasiasa wajasiri kama vile mbunge wa kiharu , Ndindi nyoro, Mohamed Ali,Aden Duale,Seneta Irungu kang’ata,Kithure kindiki, Susan kihika na kadhalika ambao wanaweza kuwashambulia mahasimu wao bila kuogopa.

Ni Kinaya kwa Dkt Ruto kuwafokea magavana hao akiwa kaunti zao, matamshi ya kejeli yatamsawiri kama kiongozi mjeuri,katili,dikteta anayepaswa kuogopwa kwa kutovumilia wakosoaji wake.Huwezi kupuuza ushawishi wa kiongozi mkakamvu kama Kiraitu Murungi na utarajie kupata ungwaji mkono kisiasa katika meru,malumbano hayo yatavuruga ushawishi wa mgombeaji huyo wa UDA na itakuwa pigo la kisiasa.

Ikiwa Naibu Rais atashindwa kupima matamshi yake na kuwa mnyenyekevu kwa viongozi wengine siamini akifaulisha ndoto yake kuwa Rais wa tano wa nchi hii.Anafaa kuelewa japo viongozi anaowasuta kwa kuvumisha Raila odinga, wengine wafuasi wao huenda wanaunga azma yake kuwa Rais , nasisitiza kuna wafuasi sugu wa Kiraitu Murungi katika juhudi zake kusaka ugavana kipindi cha pili,ila wanaunga Ruto kuwania Urais.

Je, Wafuasi kama hao wadhani watavutiwa na matamshi na bezo za Dkt Ruto dhidi ya kiongozi wao?Dkt William Ruto atanufaika pakubwa ikiwa atajenga ungwana na heshima katika kampeni zake.anapaswa kubadilisha mienendo na msimamo Wake kuhusu wakosoaji wake,asipotahadhari na kukoma kuwadunisha viongozi hao ngomeni zao atajikuta kwenye mabadiliko makubwa yatakayovuruga umaarufu wake pakubwa kabla ya uchaguzi wa 2022

You can share this post!

KPA yavizia Equity na kuponyoka na ‘mali’

Wasomali 4 wanaswa UG

F M